Home » » MREMBO WA UMBO NAMBA NANE KUSAKWA IRINGA.......................

MREMBO WA UMBO NAMBA NANE KUSAKWA IRINGA.......................

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, January 21, 2010 | 3:39 AMMSANII nguli wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Daz Baba ijumaa (tarehe 22/1/2010) anataraji kufanya onyesho kali la kufungua mwaka 2010 kiburudani ndani ya mkoa wa Iringa kwa kumsaka mrembo wa umbo namba nane ambaye atamzawadia kitita cha shilingi 100,000.

Pamoja na msanii huyo wasanii wengine ambao wamekuja mjini Iringa kufanya onyesho hilo la kuzindua mwaka 2010 kiburudani na Radio Ebony FM (87.5) ndani ya ukumbi wa V.I.P ni pamoja na mabingwa wa unenguaji sebene maarufu kwa jina la Chitu Tigo.

Akizungumza na mtandao huu , mratibu wa onyesho hilo Edwin Bashir alisema kuwa lengo la kuwaleta wasanii hao ndani ya mkoa wa Iringa ni kutaka kuufungua mwaka 2010 kuburudani na kuuaga mwaka 2009 ambao ulitawaliwa na burudani mbali mbali zilizosababishwa na kituo cha Radio Ebon Fm .

Alisema kuwa kituo hicho cha Radio Ebon Fm mbali ya kutimiza malengo yake ya kila siku kwa wasikilizaji wake ikiwa ni pamoja na kuwapa habari na elimu bado suala la burudani limekuwa likipewa nafasi yake kwa wapenzi wa burudani.

Hivyo alisema kuwa katika ukumbi huo wa kisasa wa V.I.P wasanii hao wanategemea kufanya onyesho la nguvu pamoja na kutoa zawadi kwa mrembo wa umbo namba nane ambaye atakwenda sanjari na wimbo wa msanii Daz Baba .

Hata hivyo alisema onyesho hilo mbali ya kufungua mwaka 2010 kiburudani pia litautambulisha rasmi ukumbi huo wa kisasa wa V.I.P ambao upo chini ya mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Taifa Chiku Abwao.

Mratibu huyo alisema katika kuhakikisha wadau wote wa wasanii hao wanapata kuona burudani hiyo Radio Ebon Fm imetoa ofa maalum kwa watu 100 wa kwanza ambao wataingia kwa kiingilio cha shilingi 3000 na wanafunzi wa vyuo vikuu ambao watakwenda na vitambulisho vyao wataingia kwa shilingi 2000 wakati watu wengine wote watatakiwa kulipa shilingi 4000.
MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA