Home » » MIUJIZA YA MWAKA MWANAMKE ATEKETEA KWA MOTO HADI KUFA BILA NGUO KUSHIKA MOTO.................

MIUJIZA YA MWAKA MWANAMKE ATEKETEA KWA MOTO HADI KUFA BILA NGUO KUSHIKA MOTO.................

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, January 18, 2010 | 10:35 AM

Na Francis Godwin,Iringa

MWANAMKE mmoja mkazi wa kijiji cha Welu wilaya ya Iringa vijijini Bibi Tulimndege Mwilongo (70) amefariki dunia kwa kuungua mwili mzima kwa moto wa kimiujiza ambao haukuunguza nguo wala kitanda ambacho alikuwa amelalia zaidi ya kuunguza mwili wake.

Akielezea undani wa tukio hilo ndugu wa marehemu huyo John Mwilongo alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 4 usiku wakati mama huyo akiwa amelala chumbani kwake.

Alisema kwa kawaida katika chumba chake amekuwa akilala peke yake na kuwa siku hiyo walisikia mwanamke huyo akipiga kelele za kuomba kuokolewa motoni hali iliyopelekea majirani kuamka wakiwa na maji kwa ajili ya kuzima moto ambao hata hivyo ulikuwa hauonekani .

"Wananchi wengi walijitokeza kutaka kumwokoa mama yetu ila ...ukweli moto huo alikuwa akiuona yeye peke yake watu wengine wote tulikuwa hatuoni moto ukiwaka "

Alisema kuwa kutokana na kulalamika kuungua moto huku akiwa kitandani ndipo wananchi walipoamua kumvuta kutoka kitandani wakidhani labda alikuwa akiota ndoto ila bado aliendelea kulalamika hadi alipotolewa ndani ya nyumbani hiyo.

Hata hivyo alisema baada ya kutolewa nje ya nyumba hiyo na kuwekwa kando kando ya barabara ndipo walipojaribu kumchunguza waliweza kuona majeraha makubwa ya moto mwilini mithiri ya mtu aliyeungua kwa moto wa kuni japo nguo zake hakuna hata moja iliyokuwa imeungua wala kushika moto.

" Ukisikia mauza uza ndio haya yaani binadamu mwili wote umeungua na kubaki mkaa ila nguo hazijaungua hata kidogo "

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa (ACP) Evarist Mangalla amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa hakuna mtu yeyete anayeshikiliwa wala kuhisiwa kuhusika na tukio hilo la aina yake .

Kamanda Mangalla alisema kuwa pamoja na uchunguzi wa kitaalam kubaini kuwa mwili wa mwanamke huyo umeungua kwa moto ila mazingira ya kuungua bado yanatatanisha.

Wakati huo huo watu wasiofahamika wamemchinja mkazi wa kijiji cha Ukelewe wilaya ya Mufindi Thospelina Mkakanzi (70) na mwili wake kuutupa porini .

Kamanda Mangalla alisema kuwa mwili wa mkazi huyo ulikutwa juzi majira ya saa 2 asubuhi huku ukiwa na majeraha yaliyotokana na kuchinjwa na kitu chenye ncha kali na mtu ama watu wasiofahamika na kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi.

wakati huo huo sakata la Mzee Richard Lipambile mkazi wa kata ya Imalinyi Njombe ambaye alitekwa na bado kupatikana hadi sasa limefikishwa kwa kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa na ameahidi kuingilia kati mwenyewe .

Mzee huyo alitekwa na watu walijifanya askari polisi wa kituo cha Njombe toka Desemba 23 mwaka jana na hadi sasa suala hilo limekuwa likizungushwa na polisi Njombe hadi watoto wa mzee huyo walipoamua kutinga kwa kamanda wa polisi mjini hapa ,habari kamili utaipata katika mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ama sikiliza Mornig Talk Show ya Ebon FM kwa undani zaidi wa sakata hili .
Bonya hapa

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA