Home » » MGOMBEA UBUNGE AWATOZA KINGILIO WAPIGA KURA WAKE KWENDA KUMWONA 'LIVE' MWANDISHI KITENGE NA KUMSIKILIZA YEYE......................

MGOMBEA UBUNGE AWATOZA KINGILIO WAPIGA KURA WAKE KWENDA KUMWONA 'LIVE' MWANDISHI KITENGE NA KUMSIKILIZA YEYE......................

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, January 10, 2010 | 11:22 AM


MASHINDANO ya kombe la Krismasi na mwaka mpya yaliyoanzishwa na katibu mkuu wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) Frederick Mwakalebela katika jimbo la Iringa mjini kwa ajili ya kujitangaza kugombea ubunge kupitia CCM yameingia dosari baada ya kamati ya kombe hilo kuwatoza mashabiki kiingilio cha shilingi 1000 kwa ajili ya kuingia uwanjani kumwona mtangazaji wa ITV Maulid Kitenge ambaye hakufika uwanjani hapo.

Kamati hiyo ya mashindano hayo iliyoongozwa na kundi la baadhi ya vijana wa chama cha mapinduzi (UV CCM ) likiongozwa na katibu wa kamati hiyo Shukuru Luhambati ndiyo ambayo inadaiwa kuweka kiingilio hicho pamoja na Mwakalebela kudhamini mashindano hayo kwa asilimia 100 ili watu watape burudani hiyo.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia wapenzi wachache wa soka na sanaa katika Manispaa ya Iringa wakiwa nje ya lango la kuingia uwanja wa Samora kwa kukosa kiingilio hicho cha shilingi 1000 huku baadhi yao wakihoji utaratibu wa wana CCM kuwatoza wananchi wananchi wanapokwenda kuwasikiliza.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi John Sanga , diwani kata ya Ilala Grevas Ndaki ,mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Abed Kiponza walisema kimsingi kamati hiyo imemvurugia kabisa Mwakalebela kwa kuwatoza wananchi kiingilio kwa ajili ya kwenda kumsikiliza.

Alisema Kalinga kuwa Mwakalebela alikuwa na nafasi nzuri ya kujitangaza kupitia michezo hiyo iwapo kamati ya mashindano hayo isingeendekeza njaa na kuwatoza wananchi kiingilio katika michezo hiyo.

"Katika uwanja huo huo kulikuwa na mashindano ya kombe la Iringa yetu .....mashindano yaliyokuwa na mvuto mkubwa kuliko hayo ambayo yaliandaliwa na mmoja kati ya wagombea ubunge jimbo hili...ila watu waliingia bure lakini haya ambayo yamedhaminiwa na kiongozi mkubwa wa TFF watu tunamchangia tena fedha....hii haijapata kutokea katika siasa za Tanzania kwa wananchi kulipia kwenda kumsikiliza mgombea"

Alisema kuwa kamati hiyo ilikuwa imetangaza mji mzima wa Iringa kupitia gari ya matangazo pamoja na kuandika katika ubao wa matangazo kuwa katika kuhitimisha michezo hiyo wasanii mbali mbali watakuwepo kama TMK wanaume halisi,Mrisho Mpoto,muigizaji wa sauti za viongozi Steve Nyerere na mtangazaji Maulid Kitege na kuwa kiingilio wakubwa na watoto wote shilingi 1000 na kuwa burudani hizo zingeanza majira ya saa 4 asubuhi.

Hata hivyo alisema anashangazwa hadi saa 3 katika uwanja huo ni watu wasiozidi 20 ndio walikuwa wameingia ndani ya uwanja kutokana na kugoma kulipa kiingilio cha kumwona Kitenge na kundi lake.

" Hivi hadi saa hii saa tisa hakuna msanii hata moja aliyefika huku jukwaa likiendelea kujengwa .....hivi hawa jamaa sio wamekuja kutuingiza mjini ...pia wanasema kumwona Mwandishi ni fedha mbona waandishi hapa Iringa tunao wengi sana kwani Kitenge ni msanii kweli wametufanya washamba sana"

Kwa upande wake Kiponza na Ndaki walisema kuwa utaratibu wa kuandaa michezo ni mzuri katika kutangaza chama ili ilipendeza baadhi ya vipingamizi kuondolewa ili kutoa burudani kwa wana Iringa.

Mbali ya dosari hiyo pia dosari nyingine iliyojitokeza katika mashindano hayo ni baada ya madiwani walioalikwa kufika katika mashindano hayo kushindwa kufika uwanjani hapo mbali ya kupewa mialiko .

Mmoja kati ya madiwani aliyefika uwanjani hapo alisema wengi wameshindwa kufika kutokana na kutoikubali kamati ya maandalizi ya mashindano hayo na kuwa Mwakalebela alikuwa na lengo nzuri japo kamati hiyo imemwingiza katika mkenge jambo tayari limemtia doa kwa wananchi wa Iringa mjini .

Hata hivyo kutokana na wananchi kushindwa kuingia uwanjani hapo na viongozi wa chama cha soka Manispaa ya Iringa kuwa mbali na mashindano hayo Mwakalebela aliagiza geti lifunguliwe baada ya kuona watu wachache hadi majira ya saa 9.45 alasiri.

Kwa upande wake mratibu wa kombe la Muungano Mufindi Daud
Yasin ambaye ndiye alilazimika kuwa mgeni rasimi katika fainali ya mashindano hayo alimpongeza Mwakalebela kwa kubuni mashindano hayo mjini Iringa.

MWISHO

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA