Home » » MCHIMBA MTORO WA MAJI ACHIMBUA MIFUPA YA BINADAMU................

MCHIMBA MTORO WA MAJI ACHIMBUA MIFUPA YA BINADAMU................

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Wednesday, January 13, 2010 | 8:43 AM


VIJANA wanaofanya kibarua cha kuchimba mtoro katika kampuni ya JR inayofanya kazi ya usambazaji wa mabomba ya maji safi katika katika manispaa leo walikutana na mauza uza baada ya kuchimbua mifupa ya binadamu anayesadikika kufa zaidi ya miaka 50 iliyopita.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi aliyefika eneo la tukio katika mtaa wa Frelimo magengeni vijana hao Mkombozi Msungu na Patrick Sanga ambao ni vibarua wa kampuni hiyo ya JR ,walisema kuwa mifupa hiyo ilianza kuonekana toka juzi majira ya asubuhi wakati wakichimba mtaro huo wa kupitisha mabomba ya maji safi.

Alisema Msungu kuwa akiwa na mwenzake huyo Sanga wakichimba mtaro huo walijikuta wakipitwa na mshangao mara baada ya kuchimbua fuvu la kichwa cha binadamu na baada ya muda kukutana na mbavu na miguu .

Hata hivyo alisema kuwa kutokana na mauza uza hayo walilazimika kusimama kwa muda na siku iliyofuata ambayo ni jana bado waliendelea kukutana na mifupa ya binadamu katika eneo hilo ,mifupa ambayo ilikuwa imekaa ovyo ovyo mithiri ya mtu kuirundika eneo hilo.

“kama lingekuwa ni kaburi tungeweza kutambua haraka sana ila jinsi mifupa hii ilivyokutwa inaonyesha mtu huyo alitupwa eneo hili bila kuzikwa kwani ni mita kama moja tu ndio ambayo mifupa hii ilianza kuonekana …..sasa ni kaburi gani la mita moja…hii nasema ni kali ya mwaka”

Hata hivyo alisema kuwa toka wameanza kufanya kazi hiyo ya kuchimba mitaro ni zaidi ya miezi mine sasa na hawajapata kukutana na mauza uza kama hayo na kuwa kwa upande wao hilo ni tukio la kwanza kukutana nalo .

Alisema Msungu kuwa eneo hilo la mtaro lipo ni ukingoni mwa banda la biashara za mitumba ambalo linatumiwa na kijana mmoja ambaye aliwashauri kupindisha mtaro huo ili kukwepa kuendelea kuchimbua mifupa hiyo.

Mfanyabiashara Emanuel Kaunde alisema kuwa kwa upande wake alijenga banda hilo la nguo ambalo lipo ukingoni mwa nyumba ambapo aliomba kwa wamiliki wa nyumba hiyo kujenga na kuwa eneo hilo halikuwa na na kaburi na kuwa kwa upande wake anashangaa kuona mifupa hiyo .

Mmiliki wa nyumba hiyo Antony Chonya alimthibitishia mwandishi wa habari hizi kuwa toka nyumba hiyo inajengwa na wazazi wake kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita hapajapata kuwa na kaburi wala eneo la kuzika watu zaidi ya eneo hilo awali kuwa ni pori .

Hivyo alisema yawezekana kabisa mtu huyo aliuwawa ama alipotea na kufunikwa na tope bila mtu kujua.

“ Mifupa hii baada ya kuonyeshwa tuliikusanya na kuiweka katika mfuko wa Rambo ….japo walioichimbua walitaka kuifukia tena baada ya kupitisha bomba”

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa (ACP) Evalist Mangalla alipopigiwa simu na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na tukio hilo alisema bado alikuwa hajapata taarifa na kuahidi kulifanyia kazi kwa kutuma askari kwenda eneo la tukio.

Bonya hapa

Share this article :

+ comments + 1 comments

January 20, 2010 at 1:51 AM

ni blog nzuri but pangilia vizur jinsi ya kuandika maneno haina haja ya kuandika maneno makubwa,then page moja habar moja.pia kila muda uende kwenye older post,hii haijakaa njema.nimeipenda kwa habari motomoto.keep it up!

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA