Home » » MBUNGE MSOLLA AWALISHA WALI WAPIGA KURA WAKE, MWAMOTO ALALAMIKA..............

MBUNGE MSOLLA AWALISHA WALI WAPIGA KURA WAKE, MWAMOTO ALALAMIKA..............

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, January 10, 2010 | 11:17 AM

WAKATI mbunge wa jimbo la Kilolo na waziri wa mawasiliano Sayansi na Teknolojia Profesa Peter Msolla jana (January 9) ameukaribisha mwaka 2010 kwa kufanya sherehe kubwa ikiwa ni pamoja na kuwalisha wali na vinywaji baadhi ya wapiga kura wake ,aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Venanci Mwamoto asema haungi mkono mbunge utaratibu kutoa wali

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi baada ya kumalizika kwa sherehe hizo zilizofanyika nyumbani kwa mbunge huyo eneo la mazombe Ilula ,baadhi ya viongozi wa CCM kata za jimbo la Kilolo walisema kuwa ,Mbunge Msolla amekuwa na kawaida kuandaa chakula kila January mosi toka alipoingia madarakani mwaka 2005 kama njia ya kusherekea mwaka mpya na wapiga kura wake.

Hata hivyo walisema kuwa katika sherehe hiyo waalikwa ni baadhi ya wananchi ,viongozi wa kata ,vijiji ,tarafa na wilaya kutoka maeneo yote ya jimbo hilo ambapo mbuge aliwatafutia usafiri wa kwenda na kurudi.

Hivyo walisema kuwa utaratibu huo pia umekuwa ukitumika kama njia ya kupeana majukumu ya kazi na kutathimini shughuli za maendeleo katika jimbo hilo .

Viongozi hao walisema kwa upande wao wanampongeza mbunge huyo kwa uamuzi utaratibu huo wa kula pamoja.

Wakati viongozi hao wakimpongeza mbunge Msolla kwa wema wake wa kuwapa chakula ,Mwamoto ameonyesha kupinga uamuzi huo kuwa si wa kimaendeleo na kusema kuwa mbunge huyo alipaswa kuuaga mwaka kwa kushiriki na wananchi shughuli ya kimaendeleo kama kupanda miti na baada ya kazi hiyo ndipo wangeweza kula chakula cha pamoja.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu jana Mwamoto alisema kuwa hivi kuna kwa upande wake haungi mkono hatua ya mbunge huyo kulisha wapiga kura wake wali na kuwapa pombe.

Kwani alisema jimbo la Kilolo bado lina matatizo mbali mbali ambayo yangeweza kutatuliwa na fedha hizo zilizotumika kwa kulisha viongozi chakula .

"Ujue sherehe hizo zimetumia zaidi ya shilingi milioni 4 ukiangalia fedha hizo ni nyingi sana zingeweza kununua hata madawati ya wanafunzi wa shule mojawapo ama kununua mbegu za mazao kwa ajili ya wananchi kulima....huu si wakati wa wananchi kurubuniwa kwa pombe ama wali ni wakati wa kurubuniwa kwa maendeleo"

Hata hivyo Mwamoto alisema utaratibu uliotumika wa kuwapa chakula wapiga kura wake bado wa kiubaguzi kwani waliofika kula chakula ni wale walipewa kadi maalum za mialiko na si vinginevyo jambo ambalo kwake analipinga kwani waliomchagua ni wananchi wote iweje katika chakula wanatengwa.

"Hivi hapa mhesimiwa mbunge anataka kuwaeleza nini wananchi wa jimbo la Kilolo....kama katika chaguzi wananchi wote walishiriki kumchagua na katika maendeleo wote wanashiriki iweje katika chakula wachaguliwe baadhi na wengine watengwe" alihoji Mwamoto

Kuwa ni vizuri wana Kilolo kuanza kujiuliza sasa ili kuangalia kama wanataka mbunge wa kumchagua na baada ya kumchagua kwenye neema kubaguliwa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) mkoa wa Iringa Mwigongo Kapwani aliwataka wananchi Kilolo na wilaya nyingine za mkoa huo kuepuka kununuliwa kwa wali na pombe na badala yake kufanya maamuzi sahihi katika uchaguzi mkuu mwaka huu .

Alisema kuwa hivi sasa kila mbunge na kila diwani anaweka mikakati ya kuwarubuni wapiga kura kwa zawadi ndogo ndogo wakati miaka minne yote alikuwa mbali na wananchi wake.

Kapwani alisema Chadema Iringa imepania kwa nguvu zote kulichukua jimbo hilo la Kilolo hata kama mbunge wake ameanza kutoa wali na pombe wao lazima jimbo hilo na majimbo mengine mawili katika mkoa huo kuchukuliwa katika uchaguzi huu.

" Nawaombeni sana wananchi jitokezeni kwa wingi katika ofa za chakula na pombe zinazotolewa na wagombea wa CCM ila kura zenu zote Chadema"
Kwa upande wake mbunge Msolla akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kuhusiana na sherehe hizo alisema kuwa suala la sherehe amekuwa akilifanya hata kabla ya kuwa mbunge wa jimbo hilo hivyo si mara yake ya kwanza kuwaalika wakazi wa Kilolo katika chakula cha pamoja.
Mbunge Msolla alisema kuwa kimsingi sherehe hiyo ya kuukaribisha mwaka 2010 ilipaswa kufanyika January mosi ila kutokana na Taifa kupatwa na msiba mkubwa wa mzee Rashid Kawawa alilazimika kusogeza mbele.
Hata hivyo Msolla alisema kuwa sherehe hizo ni za kawaida ambapo taasisi na watu mbali mbali wamekuwa wakifanya kuanga mwaka na kuwa bado wananchi wa jimbo hilo wanayonafasi ya kuendelea kutoa ushirikano wao katika shughuli za kimaendeleo.
MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA