Home » » MAFULIKO YATINGA NYUMBANI KWA MBUNGE LUKUVI KAYA ZAIDI YA 15 HAZINA MAKAZI ............

MAFULIKO YATINGA NYUMBANI KWA MBUNGE LUKUVI KAYA ZAIDI YA 15 HAZINA MAKAZI ............

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, January 25, 2010 | 8:58 AM


HUKU wakazi wa Tarafa ya Idodi wakiwa bado hawajasahau tukio la vifo vya wanafunzi zaidi ya 10 wa sekondari ya Idodi vilivyotokana na bweni kuungua moto ,mvua kubwa zilizonyesha kwa zaidi ya masaa manne usiku wa kuamkia leo katika tarafa ya Idodi wilaya ya Iringa vijijini ambako ni nyumbani kwa mbunge wa jimbo la Ismani mheshimiwa Wiliam Vangimembe Lukuvi mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam zimejikuta katika mkasa mwingine baada ya mafuliko kusomba nyumba zaidi ya 15 katika kijiji cha Idodi Baadhi ya familia zilizokumbwa na tukio hilo wakizungumza na mwandishi wa habari hizi jana walisema kuwa tukio hilo lilianza kutokea kuanzia majira ya saa 8 usiku wakati wakiwa wamelala.

Walisema kuwa kutokana na mvua hizo kunyesha mfululizo ilipelekea mfereji uliopo jirani na makazi yao ambao umekuwa ukitumiwa kwa shughuli za umwagiliaji kufulika maji ambayo baadae yalizagaa katika makazi yao.

Walisema kuwa kutokana na mafuliko hayo walilazimika kutoka nje huku baadhi yao wakitumia vitanda kama walivyokuwa wanatumia kulalia kama mitumbwi .

Pia walisema kuwa baadhi ya vitu vilivyo kuwemo ndani ya nyumba hizo zimesombwa na mafuliko .

Kwa upande wake afisa mtendaji wa serikali ya kijiji hicho Ignasy Kwangoliro alisema kuwa sehemu kubwa ya familia zilizokumbwa na mafuliko hayo zimehifadhiwa kwa majirani .

Alisema kuwa mbali ya vyombo kusombwa na mafuliko pia mifungo kama kuku ,bata na mbuzi zimesombwa na mafuliko hayo.

Afisa mtendaji huyo alisema kijiji hicho kilichokumbwa na mafuliko ni nyumbani kwa mbunge wa jimbo la Ismani na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Lukuvi .

Pia alisema eneo hilo la kijiji cha Idodi Tarafani ni eneo ambalo sehemu kubwa ni tambalale hivyo kila suala la mafuliko limekuwa likijitokeza mara kwa mara pindi mvua zinaponyesha zaidi.

Afisa mtendaji huyo alisema tayari viongozi wa serikali wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Aseri Msangi wameweza kufika katika kijiji hicho kuwajulia hali wananchi waliokumbwa na mafuliko hayo.

Mbunge wa jimbo la Ismani Lukuvi akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu jana kuhusiana na tukio hilo ,mbali ya kutoa pole kwa familia zilizokumbwa na tukio hilo bado alisema kuwa jitihada mbali mbali zinafanywa ili kusaidia familia zilizokumbwa na mafuliko.

Lukuvi alisema kwa upande wake amepata tarifa hiyo kupitia viongozi wa kijiji hicho na tayari amefika mkoani Iringa kwa ajili ya (leo) kwenda kuwatembelea wananchi hao.

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa sana tukio hili na sasa nipo mjini Iringa ....kesho asubuhi na mapema nitakwenda kuwajulia hali pamoja na kujua madhara zaidi yaliyojitokeza katika eneo hilo"


Mheshimiwa Lukuvi alisema pamoja na kujua madhara hayo bado atafika kutoa misaada mbali mbali kwa wahanga wa tukio hilo mapema leo na kuwaomba wasamaria wema zaidi kuendelea kujitokeza kuwasaidia wakazi hao.


matukio zaidi ya mafuliko Idodi utayapata kesho katika mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com ama waweza kusikiliza kesho asubuhi kipindi cha Morning Talk Show ndani ya radio Ebony Fm 87.8 ama 88.2 kwa mikoa ya Mbeya pia waweza kupata ndani ya wapo radio Fm kwa wakazi wa Dar
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA