Home » » KAPWANI AMSHINDWA LUKUVI ISMANI AJITOSA KWA MBEGA...................

KAPWANI AMSHINDWA LUKUVI ISMANI AJITOSA KWA MBEGA...................

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, January 19, 2010 | 11:41 AM

Na Francis Godwin,Iringa

MWENYEKITI wa chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) mkoa wa Iringa Ben Mwigongo Kapwani (52) ametangaza kugombea ubunge jimbo la Iringa mjini linaloongozwa na Monica Mbega (CCM) na kuwaomba wananchi wa jimbo hilo kumuunga mkono bila kujali itikadi zao za vyama.

Kapwani ambaye mwaka 2005 aligombea ubunge jimbo la Ismani linaloongozwa na mbunge Wiliam Lukuvi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa katika uchaguzi huo ameona ni vyema agombee jimbo la Iringa mjini ambako ni nyumbani kwake.

Akizungunza mtandao huu Kapwani ambaye ni mwana taaluma wa masuala ya udaktari na uongozi alisema kuwa mwaka 2005 alilazimika kwenda kupambana na Lukuvi Ismani baada ya kuona hakuna chama cha upinzani abacho kilikuwa kimejitokeza kuweka mgombea katika jimbo hilo.


Hivyo alisema kutokana na hivi sasa Chadema kuwa na mpango wa kuweka mgombea katika jimbo hilo kwa upande wake ameamua kuja kugombea katika jimbo la Iringa mjini ambako ni nyumbani kwake na mgombea ambaye aligombea mwaka 2005 kupitia Chadema Mashaka Tagalile alijiunga na CCM kabla ya kufariki dunia.

Pia alisema mwaka 2005 chadema ilishika nafasi ya tatu ikifuatiwa na TLP na kuwa jitihada mbali mbali zimefanywa na Chadema kuhakikisha wanajijenga vizuri ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wanachama kutoka CCM na baadhi yao wamejiunga kutoka vyama vya upinzani akiwemo aliyekuwa mgombea ubunge wa TLP mchungaji Peter Msigwa .

Hivyo alisema kuwa nguvu hiyo ya wanachama kutoka CCM na vyama vya upinzani inaweza kabisa kukiwezesha Chadema kuchukua jimbo la Iringa mjini katika uchaguzi mkuu unaotaraji kufanyika mapema mwaka huu.

Akielezea kuhusua mikakati yake baada ya kumpokea ubunge mbunge wa CCM kuwa ni pamoja na kuhakikisha wakazi wa mkoa wa Iringa hasa Manispaa ya Iringa wananufaika na uwepo wa vyuo vikuu,wanawake wanaondolewa manyanyaso makubwa wanayopata katika taasisi zinazotoa mikopo mjini Iringa kwa kuanzishiwa Benki ya wanawake itakayotoa mikopo ya riba nafuu pamoja na kuhakikisha kuna kuwpo na kiwanda kitakachosaidia kuongeza ajira kwa wakazi wa mkoa wa Iringa.


Alisema jimbo la Iringa lina kinu cha taifa cha usagishaji ambacho kwa miaka mingi sasa kimekuwa hakifanyi kazi jambo ambalo wao kama Chadema watahakikisha kinu hicho kinatumika kwa faida ya wakazi wa manispaa ya Iringa.


Hata hivyo Kapwani alieleze kusikitishwa kwake na wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuacha ofisi zao na kukimbilia kugombea ubunge ndani ya CCM.
Kuhusua mchungaji Msigwa ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho ngai ya wilaya ya Iringa mjini kutaka kugombea ubunge kupitia Chadema katika jimbo hilo ,mwenyekiti kuwa ni haki ya kila mwanachama mwenye sifa kuomba kuchaguliwa na kushiriki kuchagua viongozi hivyo hamkatazi mwanachama yeyote kujitokeza kugombea.


"Chama chetu kinaendeshwa kwa demokrasia hivyo ....kutangaza mimi kugombea sio kwamba nawakataza wengine kujitokeza naomba wana Chadema wote wenye sifa waweze kujitokeza kugombea...ila naomba ieleweke wazi kuwa sio mimi napingana na Msigwa katika jimbo la Iringa mjini kwani mwaka 2005 Msigwa alikuwa mgombea wa TLP sio Chadema na sasa amerudi chadema tunamkaribisha kuungana na wachama wengine kuomba nafasi za uongozi rukrsa vikao vya wanachama na wananchi ndio watakaotoa uamuzi "
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA