Home » » DAZ BABA AMAVAA JK ,ATOA ONYO KALI KWA WASANII WENZAKE

DAZ BABA AMAVAA JK ,ATOA ONYO KALI KWA WASANII WENZAKE

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, January 24, 2010 | 3:23 AM

MSANII maarufu hapa nchini wa muziki wa kizazi kipya David Jacob a.k.a Daz Baba Mwalimu amemvaa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumtaka kuwabana COSOTA ili wasanii waweze kunufaika zaidi .

Pia msanii huyo ametoa onyo kali kwa wasanii watakaotumiwa na vyama vya siasa katika kampeni za uchaguzi mkuu kuepuka kuwa chanzo cha kuchochea vita kwa kwatanzania kwa kutunga nyimbo za kampeni zinazo jenga chuki kwa vyama vingine ama kwa watanzania .


Msanii huyo amemwomba Rais Jakaya Mrisho Kikwete kukumbuka ahadi yake kwa wasanii ya kuwaendeleza ili kujulikana zaidi katika nafasi za kimataifa badala ya ilivyo sasa.

Sehemu kubwa kazi zetu zimekuwa zikipigwa bila ya sisi kunufaika mfano ukienda katika mitandao utaona watu wanatazama bure kazi zetu ila bado COSOTA wanasema wanafanya kazi .

Msanii huyo alitoa onyo hilo wakati akizungumza na mtandao huu mara baada ya kumaliza onyesho lake la kumsaka mrembo mwenye umbo namba nane katika ukumbi wa Club V.I.P mjini Iringa .

Mbali ya kuwapongeza watanzania kwa kuendelea kuwakubali wasanii mbali mbali hapa nchini ila bado amewataka watanzania kuepuka kukubali kuingizwa katika uhasana na wasanii wasio penda amani ambao wataingia mikataba na baadhi ya vyama vya siasa kwa ajili ya kuhamasisha chuki baina yao na chama kingine ama kundi la watu furani .

Kwani alisema Tanzania ni nchini yenye amani na utulivu na ndio sababu hata wao kama wasanii wamekuwa wakifanya maonyesho yao kwa uhuru na amani na kuimba nyimbo zozote bila kukatazwa na mtu.

Hivyo alisema pamoja na watanzania kuendelea kuheshimu kazi za wasanii ila bado wasanii wenyewe wanayo nafasi kubwa ya kujiheshimu na kuheshimu amani iliyopo na hata kama wataingia mikataba na vyama vya siasa wasikubali kutumiwa kuvuruga amani iliyopo .

"..wasanii tuna heshimiwa sana na jamii inayotuzunguka hivi leo hata ukitoka na nyimbo isiyo eleweka bado ukipeleka dukani itanunuliwa ...sasa tusikubali kujivunjia heshima hii lazima tulinde amani kwani kama tunachangia viongozi wabovu kuingia madarakani athari zake kwetu sote"

Daz Baba alisema kuwa kipindi cha kampeni kimefika na baadhi ya vyama vimekuwa vikipenda kuwatumia sana wasanii katika kampeni ila bado wasanii wasikubali kutumiwa kuvuruga amani ama kutumika bila kuwepo maslahi kwao.

Hata hivyo alisema kuwa kamwe wasanii wasikubali kupoteza heshima yao kwa kugeuzwa watumwa ama madaraja ya wanasiasa katika kampeni .

Hivyo alisema si jambo jema kwa wanasiasa kuwageuza wasanii daraja lao na baada ya hapo wamekuwa wakiwaacha bila kuwahudumia.

"Mimi kama Rasta nakataa utumwa napenda amani .....hivyo sipo tayari kutumika kumwaga damu za watanzania kwa sanaa yangu .... nipo tayari kulinda amani ya watanzania kupitia sanaa yangu"

Kuhusu COSOTA alisema kuwa chombo hicho kwa sehemu kimepoteza mwelekeo na wasanii wamekuwa hawanufaiki chochote na chombo hicho na kumwomba Rais Kikwete kuangalia namna ya kuboresha chombo hicho kabla ya uchaguzi mkuu.

Akitolea mfano alisema kuwa wasanii wa nje wamekuwa wakiheshimiwa na kulipwa ujira mzuri kuliko wasanii wa ndani ambao wamekuwa wakiishia kulipwa fedha za madafu na mhogo huku COSOTA wakiendelea kujinufaisha na wasanii hapa nchini .

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA