Home » » ASKARI POLISI MAFINGA WAVUNJA NGOME YA UJAMBAZI ,WANUSURIKA KUUWAWA

ASKARI POLISI MAFINGA WAVUNJA NGOME YA UJAMBAZI ,WANUSURIKA KUUWAWA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, January 28, 2010 | 11:17 AM


RPC Iringa ACP Evarist Mangalla


Askari polisi wakiangalia bunduki aina ya SMG iliyokutwa nyumbani kwa jambazi.

Na Francis Godwin,Mafinga

ASKARI polisi wa kituo cha Mafinga wilaya ya Mufindi aliyefahamika kwa jina moja la Pendo amenusurika kuuwawa kwa risasi wakati polisi wa mkoa wa Iringa wale wa mkoa wa Dodoma kuvamia na kuisambaratisha ngome ya ujambazi katika mikoa ya Iringa na Dodoma eneo la Changarawe mjini Mafinga wilayani hapa.Tukio hilo limetokea leo majira ya saa 12 asubuhi katika nyumba moja iliyopo eneo la Changarawe mjini Mafinga wakati polisi wa mkoa wa Iringa na Dodoma walipovamia nyumba hiyo ambayo ni ngome ya ujambazi kwa lengo la kutaka kumkamata kiongozi wa mtandao huo wa ujambazi katika mikoa hiyo miwili.


Wakielezea tukio hilo ambalo limeshuhudiwa pia na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com Jema Ndelwa na Hamisi Kalinga ambao ni wakazi wa eneo hilo walisema kuwa kama si askari huyo kukwepa kwa kulala chini kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kuuwawa .


Kwani walisema kuwa baada ya askari hao kufanikiwa kuizunguka nyumba hiyo jambazi hilo ambalo lilikuwa katika nyumba hiyo ambayo imekuwa ikitumika kama ngome yao liliweza kutoka huku likiwa limeiweka sawa bastola yake na kumlenga askari huyo kifuani kabla ya kukwepa.


“Kweli tunawapongeza sana askari wa Mafinga na wale wa Dodoma kwa mbinu ambayo wameweza kuitumika katika kuisambaratisha ngome hii kuu ya ujambazi katika mikoa ya Iringa na Dodoma ”


Mmoja kati ya askari ambaye alikuwepo katika msako huo ulioongozwa na mkuu wa upelelezi wilaya ya Mufindi Erick Kayombo alisema kuwa pamoja na jambazi hilo kufyatua risasi moja kwa lengo la kumpiga askari mwenzao huyo bado jamabazi hilo liliweza kutimua mbuni na kutelekeza silaha zake.


Hata hivyo alisema askari polisi Mafinga waliweza kufika eneo la tukio kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya polisi na raia wema ambao walitoa taarifa kwa mkuu wa polisi wilaya ya Mufindi (OCD) Peter Kakamba ambaye alipanga kikosi hicho kwa kushirikiana na askari wa polisi wa Dodoma ambao walifika mkoani hapa kwa ajili ya kumsaka jambazi huyo ambaye ni kiongozi wa mtandao wa ujambazi .Jambazi huyo ambaye wamemtaja kwa jina ambalo kwa sasa limehifadhiwa kwa sababu za kiusalama kutokana na kuendelea kutafutwa na jeshi la polisi ,amefanikiwa kutoroka huku akiwa na bastola moja wakati bunduki aina ya SMG ,Bastola moja ,magazeni tatu na risasi 40 zikikamatwa na jeshi la polisi .


Silaha hizo zilikutwa zimechimbiwa katika kona za nyumba ambayo ilikuwa ikitumiwa kama ngome.


Hata hivyo inadaiwa jambazi huyo mapema mwa mwezi huu alifanya ujmbazi wa kutumia silaha katika duka moja la vocha mjini Mafinga na kupora zaidi ya shilingi milioni 1


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa (ACP) Evarist Mangalla amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kuwa taarifa sahihi na hatua iliyofikiwa juu ya tukio hilo zitatolewa kwa vyombo vya habari.

MWISHO

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA