Home » » SOPHIA SIMBA AFYATUKA AWA MBOGO KWA VYOMBO VYA HABARI..............

SOPHIA SIMBA AFYATUKA AWA MBOGO KWA VYOMBO VYA HABARI..............

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, December 4, 2009 | 10:56 AMBAADA ya kimya kirefu dhidi ya tuhuma mbali mbali zinazoelekezwa kwake ,mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi Taifa (UWT) Sophia Simba amewataka wanawake kutokubali kuchonganishwa na watu wasioitakia mema CCM na kuwa tuhuma zinanazotolewa kupitia vyombo vya habari ni zakizushi na hakuna marumbano yoyote ndani ya UWT wala hakuna siku aliyomvua mwanamke yeyote nguo kikaoni.

Simba ambaye amepata mapokezi makubwa Iringa na kupopkelewa kwa maandamano ,amesema watu wasiokitakia mema chama tawala wamekuwa wakitumia njia mbali mbali kutaka kukisambaratisha na hata tuhuma mbali mbali dhidi yake zimelenga kuigawa UWT na CCM.

Bila kutaja watu hao wanaotumika kukuisambaratisha CCM kwa kuzusha tuhuma ,alisema kuwa ni vyema wanawake kmuwa makini na kuepuka kuendelea kuchonganishwa na kundi hilo la watu wenye nia mbaya ya CCM.

Simba ambaye ni waziri wan chi ofisi ya Rais utawala bora alitoa kauli hiyo leo mjini Iringa wakati akiwahutubia wanawake wa mkoa wa Iringa katika ukumbi wa jumba la maendeleo ya jamii Kitanzini.

Simba aliwataka wanawake kutoendelea kubaki pale wanapochonganishwa na kuwa ni vyema wanawake wote kujenga mazoea ya kuongea ili kukiwezesha chama kuwa na wanawake wenye uwezo wa kukisemea na kukitetea chama pale kinapozushiwa mambo ya uongo .

Kwani alisema kuwa ukimya wa wanawake ndio ambao unaweza kupelekea chama kuonekana hakifanyi chochote ila iwapo kila mwanamke ataweza kukisemea chama hata kundi hilo la watu wasio na mapenzi mema na CCM linaweza kufa lenyewe.

Alisema kuwa zipo baadhi ya nchi za magharibi ambazo zimekuwa zikikionea wivu chama cha mapinduzi kwakuwepo madarakani kwa miaka zaidi ya 40 toka nchi ilipopata uhuru wake mwaka 1961 bila kushindwa na ndio ambao wamekuwa wakiwatumia baadhi ya watu hapa nchini kwa kuelekeza tuhuma mbali mbali dhidi ya CCM na serikali yake ili kuwafanya wananchi kukichukia chama jambo ambalo si kweli na linapaswa kuepukwa na wana CCM.

Simba alisema kuwa viongozi wa serikali zote nne toka ya hayati mwalimu Julius Nyerere hadi serikali hii ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete zimeweza kufanya kazi kubwa sana katika Taifa hili na kuwa hata maendeleo haya ambayo wananchi wamekuwawakiendelea kunufaika ni matunda ya serikali ya CCM jambo ambalo baadhi ya watu wamekuwa hawapendi kuona wala kusikia .

Pia awalitaka wanawake kuanaza kuijenga CCM kutoka katika familia zao na kuwa wale ambao wana vijana wao ambao ni wana vyama wa upinzani kuhakikisha wanawabadilisha na kuwa CCM ili kuweza kukipa ushindi CCM.

Japo kuna maneno maneno ambayo yamekuwa yakijitokeza kuwa wanawake hawapendani ila ukweli wanawake wa UWT wamekuwa wakipendana na katika kuhakikisha hilo wanawake wanatakiwa kuwaonyesha wale wanaoendelea kuivuruga CCM kwa kuwapuuza.

Hata hivyo amewataka viongozi wa UWT kuepuka kuwa omba omba na badala yake kubuni miradi yao itakayowawezesha kujitegemea tofauti na ilivyo sasa ambapo wamekuwa wakitegemea kuomba omba.

Kuhusu ukomo wa madiwani wa viti maalum aliwataka kuondokana na udiwani wa viti maalum na kugombea katika kata na majimbo .

Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa na mjumbe
wa baraza kuu la UWT Taifa Bi Zainabu Mwamwindi na katibu wa UWT wilaya ya Iringa mjini Asha kalani walisema kuwa hawababaishwi na kelele zinazoelekezwa kwa mwenyekiti huyo

Mwamwindi alisema kuwa wana wanaimani kubwa na Simba na hata hao wanaopiga kelele wanajisumbua bure wao hawatamchoka wala kukatishwa tama.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA