Home » » MWAKALEBELA ATANGAZA KUNG'ATUKA TFF MWAKA 2010

MWAKALEBELA ATANGAZA KUNG'ATUKA TFF MWAKA 2010

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, December 27, 2009 | 3:51 AM


KATIBU mkuu wa shirikisho la soka Tanzania (TFF)Fredrick Mwakalebela(pichani) amesema hatakuwa tayari kuendelea kuongoza nafasi hiyo mwaka 2010 baada ya wakazi wa jimbo la Iringa mjini kumchagua kuwa mbunge wao mpya.Mwakalebela ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya michezo ya VANNEDRICK (T) Ltd alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Iringa mara baada ya kampuni yake hiyo kukabidhi udhamini wake wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 3 kwa timu zote kata 14 za jimbo la Iringa mjini kwa ajili ya ushiriki wa mashindano ya kombe la Krismasi na mwaka mpya linaloendelea katika jimbo hilo.

Alisema kuwa pamoja na kuwa muda way eye kutangaza kugombea ubunge katika jimbo hilo bado ila anamakusudi ya kufanya hivyo akiwa kama mwanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) mara baada ya muda kufika.Kwani alisema kuwa akiwa kama mtanzania katiba inampa nafasi ya kushiriki kuchagua viongozi na kuchaguliwa hivyo muda utakapofika kwa wana CCM kuanza kuchukua fomu za ubunge pia atajitokeza kufanya hivyo.Hata hivyo alisema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakihusisha udhamini wake katika mashindano hayo na harakati za yeye kugombea ubunge jimbo hilo jambo ambalo si kweli bali anafanya hivyo kama mdau wa soko mkoa wa Iringa na Tanzania .“Kuhusisha mashindano hayo na harakati zangu za kugombea ubunge si sahihi kwani lengo langu ni kuendeleza soka nchini na tayari nimefanya mashindano kama haya katika mikoa mbali mbali kama Mbeya,Mwanza ,Dar es Salaam na Tabora hivyo sijaanza hapa Iringa na kama suala la ubunge muda ukifika nitatangaza kugombea sitaogopa “Mwakalebela alisema kuwa akiwa katibu wa TFF amefanya mambo makubwa ambayo watanzania wote ni mashahidi na kuwa sasa anataka mambo hayo kuleta jimbo la Iringa mjini.Hata hivyo anasema kuwa iwapo wakazi wa jimbo la Iringa watapa nafasi ya kuwa mbunge wa jimbo hilo ataachana na shughuli za TFF na kubaki kama mdau wa soka nchini na badala yake kutumia muda wake wote kuwatumikia wananchi kama mbunge.Mwakalebela alisema kuwa suala la wabunge kuishi mbali na majimbo yake kwake kama atakuwa mbunge suala hilo halitakuwepo na muda mwingi atakuwa na wananchi na kabla ya kwenda bungeni ataweka utaratibu wa kukutana na wananchi ili waweze kumpata kero zao ambazo wangependa zifike bungeni.

Awali mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa mashindano ya kombe hilo mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi mbali ya kumpongeza katibu mkuu huyo wa TFF kwa kuonyesha nia ya dhati ya kufufua soka ndani ya Manispaa ya Iringa ,bado alisema kuwa jitihada za katibu huyo Mwakalebela zinapaswa kuendelezwa na wadau wengine.Mwamwindi alisema kuwa moja ya mambo ambayo vijana wamekuwa wakikosa katika Manispaa ya Iringa ni pamoja na udhamini wa michazo mbali mbali inayoanzishwa na kuwa kumpata mdhamini kama huyo ni ukombozi mkubwa katika sekta ya michezo mkoani Iringa.Hata hivyo alimwomba katibu mkuu huyo wa TFF nchini kuendelea kuhamasisha michezo katika Manispaa ya Iringa na mkoa na kuwa wao kama viongozi wataendelea kumuunga mkono katika suala hilo .Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya mashindano hayo Julio Elieza akisoma risala ya michezo hiyo mbele ya mgeni rasmi alisema kuwa pamoja na wao kuanzisha mashindano hayo bado suala la udhamini limeonekana kuwa tatizo na kila mdau uliyefuatwa alitoa sababu kabla ya Mwakalebela kujitokeza kudhamini mashindano hayo kwa asilimia 100.

MWISHO
Share this article :

+ comments + 1 comments

December 29, 2009 at 7:02 AM

Tunamtakia kila la kheri katika kazi yake mpya ya kutumikia wananchi ambayo anatarajia kuanza mwaka 2010 mungu akipenda.

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA