Home » » MLEMAVU MWANAFUNZI AZALISHWA NA MFANYABIASHARA NA KUKIMBIWA

MLEMAVU MWANAFUNZI AZALISHWA NA MFANYABIASHARA NA KUKIMBIWA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, December 3, 2009 | 11:04 AM


WAKATI jana ilikuwa ni siku ya maadhimisho ya watu wenye ulemavu duniani ,mfanyabiashara maarufu mkoani Iringa anadaiwa kumzalisha watoto wawili mlemavu wa viungo aliyekuwa akisoma kidato cha pili katika sekondari ya Lugalo Iringa kuhama mkoa.

Mfanyabiashara huyo anadaiwa kumdanganya mlemavu huyo kuwa angemsomesha hadi chuo kikuu iwapo na asingependa mtu yeyote hata ndugu kujua kama yeye ana mahusiano na mloemavu huyo ila baada ya kumpa mimba alihama mkoa na kukimbilia mkoa wa Arusha ambako anaendelea na biashara zake hadi sasa.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana mlemavu huyo Yolanda Mbangile (39)(pichani) mkazi wa Mwangata mjini Iringa alisema kuwa kwa sasa amekuwa akiendesha maisha yake kwa msaada wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Neema Craft ambayo imekuwa ikiwasaidia walemavu kwa elimu ya ufundi na misaada mbali mbali.

Mlemavu huyo alisema kuwa mwanaume huyo aliye mtaja kwa jina la Thadei Miho alimwachisha masomo akiwa na miaka 15 baada ya kumpa mimba .

Alisema kuwa baada ya kumpa mimba na kukimbia alilazimika kuacha masomo akiwa kidato cha pili na baada ya kuzaa mtoto alilazimika kuendelea kukaa nyumbani akijishughulisha na kazi ndogo ndogo za mikono ili kuweza kupata fedha za kusomeshea mtoto wake ambaye kwa sasa anasoma kidato cha sita .


Hata hivyo pamoja na mwanaume huyo kukimbia kuwajibishwa kisheria kwa kumwachisha masomo bado alirudi kutoka mafichoni na kumdanganya kuwa amekuja kutaka kumwendeleza kimasomo na kuonekana kwa wazazi kauli ambayo kwa upande wake ilimvutia na kumkaribisha tena .Alisema kuwa ilikuwa ni mwaka 1996 ambapo mwanaume huyo aliporejea akitokea Msoma kujificha huko kwa miaka kadhaa akikwepa kukamatwa .
Pia alisema kuwa kati ya mambo ambayo mwanaume huyo alikuwa akipinga kwa nguvu zote ni pamoja na kuonekana kwa jamii kama yeye ni rafiki na mtu mwenye ulemavu .

Alisema kuwa kila wakati alikuwa akimwomba kumtunzia siri kwa jamii ili isijue kama amezaa na mlemavu .Mwanamke huyo alisema kuwa toka amemzalisha mtoto wa pili mwanaume huyo amekimbia moja kwa moja mkoa wa Iringa na kuhamishia biashara zake mkoa wa Arusha .

Kwani alisema mbali ya mwanaume huyo kumwachicha masomo kwa kumpa mimba bado mzazi wake hakuweza kuchukua hatua zozote dhidi ya mwanaume huyo na kuwa hivi sasa baba yake ni mzee ambaye hana shughuli yeyote na amekuwa akitegemea mahitaji yake kutoka kwake.


"Hapa nilipo mimi sina mana ila baba mzima yupo kijiji cha Kaning'ombe wilaya ya Iringa lakini mimi ndiye ninayemtunza hadi sasa"

Hivyo alisema kwa upande wake pamoja na kuwa ni mlemavu anamzigo wa kutunza familia yake ya watoto wawili pamoja na baba yake huyo na baadhi ya ndugu ambao wanamtegemea


Pia alisema kuwa mbali ya kuwepo Neema Craft bado alikuwa akijishughulisha kwa biashara ya genge ambalo kwa sasa uongozi wa Manispaa ya Iringa umelivunja kwa madai limejengwa bila kufuata sheria za mipango miji .Mlemavu huyo aliiomba serikali kujaribu kutoa msaada wa mikopo ya elimu ya juu kwa asilimia 100 kwa watoto wa walemavu kama yeye badala ya ilivyo sasa ambapo anatakiwa kuchangia asilimia 40 kwa ajili ya mtoto wake kujiunga na chuo.

Aidha aliwaomba wasamaria wema ambao wapo tayari kumsaidia misaada mbali mbali ikiwemo ya elimu ya sekondari kuweza kujitokeza ili aweze kuendelea na masomo hayo ambayo ameyakosa.Aliwataka wale wote ambao wapo tayari kumsaidia kuweza kuwasiliana kwa namba 0782 45 5584 ama namba ya mwandishi wa mtandao huu 0754 026 299.

Kwa upande wake akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa sharti la kutotaja jina kwa kuwa si msemaji mkuu wa shule hiyo ya Lugalo mmoja kati ya walimu shule hapo alisema kuwa mbaWakati kwa upande wake mlemavu Claud Mahimbe na Haruna Mbata walisema kuwa kundi la walemavu limekuwa likisaulika na serikali hali inayopelekea walemavu kuendelea kuishi kwa shida kubwa.
Walisema kuwa serikali imekuwa ikiadhimisha maadhimisho mbali mbali kwa kuyapa kipaumbele ila siku ya walemavu imekuwa haipewi kipaumbele chochote jambo ambalo serikali inapaswa kutazama upya.
Kuhusu watu wanao warubuni walemavu wa kike kwa kuwapa mimba na kujificha walipendekeza kuwepo kwa sheria kali itakayowabana wale wote watakaobainika kuzaa na walemavu na kuwakimbia kama ilivyo kwa Bi.Yolanda.Kwa walisema wanaume wengi wamekuwa wakiwarubuni watu wenye ulemavu kimapenzi na baada ya kupata walichotaka wamekuwa wakiwakimbia na baadhi yao kuwataka wasijulikane na kutoa lugha za vitisho kama watawataja kwa jamii.Hata hivyo walisema wakati umefika kwa serikali kuelekeza mikakati yake kwa watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kuwajengea makazi maalum ambayo yatafahamika badala ya ilivyo sasa ambapo wengi wanaishi kwa shida na kutengwa na familia zao.


Mtaalam wa mazoezi ya viungo kwa watoto wenye ulemavu katika kituo cha Neema Craft Beatrice Swai alisema kuwa wilaya ya Iringa vijijini imekuwa ikiongoza kwa wawazi kuficha watoto wenye ulemavu jambo ambalo kwa sasa mradi wa CMS unaofadhiliwa na serikali ya Uingereza umeendelea kutoa elimu na kuwasaidia watoto hao.


Alisema kuwa toka mradi huo uanzishwe mwaka 2007 kwa kutoa huduma kwa mtoto mmoja sasa ni watoto 105 wamepatiwa mazoezi ya viungo na wanaendelea vizuri na kutoa wito kwa wazazi wa watoto wenye ulemavu kuwafichua watoto wao ili waweze kupata matibabu.
Swai alisema kuwa sababu kubwa za watoto kuzaliwa walemavu ni mamoja na wanawake wajawazito kukaa mbali na hospitali na kulazimika kujifungua katika mazingira ya shida ,kuzidishiwa dozi za tiba ya maralia pale wajawazito wanapo ugua ugonjwa huo na sababu nyingine nyingi zikiwemo za uzembe wa wauguzi.

MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA