Home » » MATOKEO DARASA LA SABA 2009,RUVUMA WATOA VISINGIZIO VYA MIUNDO MBINU.........

MATOKEO DARASA LA SABA 2009,RUVUMA WATOA VISINGIZIO VYA MIUNDO MBINU.........

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, December 11, 2009 | 9:10 AM


Baadhi ya waandishi wa habari mkoani Ruvuma wakiwa kazini,aliyevaa suti ni Adamu Nindi wa star tv,na Gerson Msigwa wa TBC-songea.,chini ni wajumbe wa kikao cha uchaguzi wa wanafunzi Ruvuma (picha na Alpius Mchucha)Kutoka mkoani Ruvuma mwandishi wa blog hii Bw.Alpius Mchucha anaripoti kuwa;
MAZINGIRA ya miundombinu kwa baadhi ya shule za sekondari mkoani Ruvuma bado hayaridhishi kutokaana na kutokamilika kwa miundombinu ya shule hizo jambo linalopelekea kutokamilika kwa malengo yaliyotarajiwa.

Kauli hiyo ilitolewa jana na katibu tawala wa mkoa wa Ruvuma,Salehe Pamba katika ukumbi wa songea clabu mjini hapa wakati akitangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka huu na uchaguzi wa wanafunzi kuingia kidato cha kwanza mwaka 2010.

Alisema ingawa mkakati wa mkoa umeweza kupeleka kidato cha kwanza kwa wanafunzi wote waliofaulu,lakini bado jitihada hizo bado zinakwamishwa na changamoto kadhaa hususani kukosekana kwa vyoo bora,majengo ya utawala,hosteli,maabara,nyumba za walimu,maktaba na upungufu wa vyumba vya madarasa.

Pamba aliwataka wadau wa elimu na viongozi wa halmashauri za wilaya mkoani humo kuhakikisha kuwa wanaboresha mazingira ya miundombinu ya shule zao na kuongeza kuwa hiyo ni mbinu mojawapo wa motisha kwa walimu na wanafunzi kwa maendeleo bora ya taaluma mashuleni,hususani katika kipindi hiki ambacho watahakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa,wanakwenda kujiunga kidato cha kwanza hapo mwakani.

Aidha awali katibu tawala huyo aliwataka wataalamu na wadau wa elimu kuhakikisha wanatekeleza mikakati iliyowekwa kwa vitendo na kitaaalamu huku akiwataka kuachana na kufanya utekelezaji wa zimamoto bali uwe wa kudumu unaolenga alama za nyakati,ili kuleta ufanisi wa kazi zao na elimu bora.

Hata hivyo akitangaza matokeo hayo Pamba alisema mkoa huo kwa mwaka 2009 ulikuwa na watahiniwa wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi wapatao 33,826,ambapo kati ya hao wavulana walikuwa 16,946 na wasichana 16,830 ambapo ni sawa na asilimia 97.2 ya watahiniwa wote waliofanya mtihani,wakati idadi ya waliosajiliwa kufanya mtihani ikiwa ni wanafunzi 34,788.

Alisema watahiniwa waliofaulu mtihani ni 18,948 ambapo wasichana ni 9,083 na wavulana 9,885,sawa na ufaulu wa asilimia 56 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani kwa mkoa mzima na kuongeza kuwa ingawa kwa matokeo hayo kuna ongezeko kidogo la asilimia 5.8 ikilinganishwa na ufaulu wa asilimia 50.2 kwa mwaka 2008.

Alizitaja wilaya zilizoongoza kimkoa ya kwanza ni halmashauri ya manispaa ya songea iliyopata asilimia 70,ikifuatiwa na halmashauri ya wilaya ya songea vijijini iliyopata asilimia 64.3,halmashauri ya wilaya ya Namtumbo iliyopata ufaulu nwa asilimia 60,halmashauri ya wilaya ya Mbinga ilyopata ufaulu wa asilimia 50.8 huku ikifunga mkia halmashauri ya wilaya ya Tunduru iliyopata asilimia 47.6 ikiwa na ongezeko la asilimia 4.8 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2008 ya asilimia 42.8.

MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA