Home » » Flag this messageManispaa ya Iringa yatumia tingatinga kuwaondoa wafanyabiashara wakakaidi wakiwemo polisi

Flag this messageManispaa ya Iringa yatumia tingatinga kuwaondoa wafanyabiashara wakakaidi wakiwemo polisi

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, December 1, 2009 | 9:20 AM

Na Francis Godwin,Iringa

WAFANYABIASHARA ndogo ndogo (machinga) walikuwa wamejenga mabanda ya biashara katikati ya barabara eneo la Posta mjini Iringa na askari waliojenga nje ya kota za polisi kinyume na sheria za mipango miji na kugoma kuondoka katika maeneo hayo wametolewa kwa nguvu baada ya uongozi wa Manispaa ya Iringa kutumia tingatinga kuvunja maeneo hayo ya biashara jana alfajiri na mapema.

Katika eneo hilo ambalo wananchi wa Manispaa ya Iringa walikuwa wakiulalamikia uongozi wa Manispaa kwa kushindwa kuwaondoa wafanyabiashara hao kwa kuwa eneo hilo wamiliki wake ni vigogo wa serikali wakiwemo watumishi wa ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa akiwemo aliyekuwamkurugenzi wa Mnaispaa hiyo Abubakari Midello ambaye aliyekuwa ofisa mipango miji wa Manispaa hiyo na viongozi wengine wa juu wa halmashauri hiyo na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudidia tingatinga la Manispaa ya Iringa likitishia kuvunja eneo hilo juzi majira ya saa 1 usiku huku baadhi ya wafanyabiashara wakiendelea na shughuli zao na kupelekea wateja kukimbia na fedha huku vibaka wakipora mali za wafanyabiashara hao baada ya shirika la ugavi waumeme nchini (TANESCO) mkoa wa Iringa kukata ghafla umeme katika eneo hilo ili kupisha zoezi lakuwaondoa wafanyabiashara hao.

Hata hivyo kutoka na umeme kukatwa ghafla katika eneo hilo na kuwashwa tena moja kati ya vibanda vya biashara katika eneo hilo kilinusurika kuwaka moto wakati mmiliki wakibanda hicho akijaribu kutoa mita ya umeme kienyeji katika kibanda chake.

Wakizungumzia hatua hiyo ya Manispaa ya Iringa ya kutumia karandinga kuwafukuza wafanyabiashara hao ,wananchi wa Manispaa ya Iringa wakiwemo wafanyabiashara walisema kuwa hatu hiyo ni nzuri japo imewaacha katika wakati mugumu zaidi kimaisha.

Samson Sanga na Selina Kalinga walisema kuwa uongozi wa Manispaa ya Iringa ulikuwaumetoa muda wa siku 21 kutoka siku ambayo walitoa notisi kwao na siku hiyo ilikuwa ikiisha Desemba 2 mwaka huu ila katika hali ya kushangaza wametolewa kabla ya siku kufika.

Alisema sanga kuwa wao hawapingi kuondolewa katika eneo hilo ila wanapinga hatua iliyotumika kuwaondoa katika eneo hilo .

Kwani alisema hadi sasa baadhi yao wamekuwa wakiendesha biashara zao kwa mikopo na kuwa kuondolewa bila kuonyeshwa eneo la kwenda ni sawa na kuwaangamiza kimaisha na kuwafanya wafungwe kwakushindwa kurejesha mikopo.

Sanga alisema kuwa kwa upande wake eneo hilo alikuwa amepanga kwa mmoja kati ya vigogo wa serikali ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa ambaye ndiye alikuwa mmiliki wa eneo hilo la biashara huku mke wake alikuwa amepanga kibanda kilichokuwa cha mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa ila vyote vimevunjwa.

"Mimi nilikuwa mpangaji tu katika eneo hili ila mbali ya kukosa eneo la kufanyia biashara napongeza sana hatua za mkurugenzi wa sasa wa Manispaa ya Iringa Terresia Mmbando kwa kutekeleza vyema majukumu yake bila upendeleo...nasema tukipata viongozi 10 kama hawa nchini ufisadi utakwisha kwa kuwa mkurugenzi huyo hajali CCM ,upinzani wala ofisi yake yeye ni sheria na yeye "

Alisema kimsingi eneo hilo lilikuwa si la biashara bali ni eneo la barabara ila watumishi wa Manispaa ya Iringa kwa wakati huo waliamua kugeuza kuwa eneo la biashara kinyume na sheria za mipango miji.

Kwa upande wake Kalinga alisema kuwa wafanyabiashara wa eneo hilo walikuwa wamechanga fedha za kuweka wakili kwa ajili ya kupinga wao kuhamishwa ila kabla ya mahakama kutoa uamuzi wake tayari wametolewa .

Pia alisema kuwa baadhi ya askari ambao wanamiliki vibanda vya biashara katika eneo hilo wamekuwa wakipinga kuondoka kwa kupitia kundi la wafanyabiashara ambao wamekuwa wakichangisha fedha na kuwa kwa sasa wanataka kuwadai fedha zao walizochanga.

Kaimu mkurugenzi waManispaa ya Iringa Juliana Letara alisema kuwa kilichofanyika katika eneo hilo ni utekelezaji washeria ya mipango miji na kuwa hata kama watakwenda mahakamani bado haitasaidia kwani wao wanatekeleza sheria .

Aidha alisema kuwa wamelazimika kuanzia kubomoa kwa wafanyabiashara ambao walikuwa wakiwadanganya wenzao wasitii agizo la Manispaa kama njia ya kutekeleza zoezi hilo na kuwa ili kuonyesha kuwa hakuna aliyejuu ya sheria ndio sababu ya kwenda kuvunja mabanda hata yale yaliyokuwa yamkimilikiwa na askari polisi eneo la kota za polisi kama njia ya kuonyesha mfano .

Mbali ya kuvunja vibanda hivyo zaidi ya 200 pia uongozi wa Manispaa ya Iringaumetoa muda wa siku 30 kuanzia jana kwa wafanyabiashara zaidi ya 20 waliosalia katika eneo hilo kuondoka .

MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA