Home » » BREAKINGNEWzzzzzzzzzzzzzzzzAJALI YAUA WATATU IRINGA

BREAKINGNEWzzzzzzzzzzzzzzzzAJALI YAUA WATATU IRINGA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Wednesday, December 9, 2009 | 9:16 AM


WATU wawili wakukufa papo hapo na wengine watatu kujeruhiwa vibaya baada ya magari matatu likiwemo basi la kampuni ya Sumry High Class lenye namba za usajili T 586 AVR Nissani kugongana katika milima ya Kitonga katika bara bara kuu ya Iringa –Dar es Salaam.

Ajali hiyo ambayo imesababishwa na dereva wa gari aina ya salon (Tax) lenye namba za usajili T 501 APX ambaye anadaiwa kuendesha gari hilo huku akiwa amelewa kupita kiasi ilitokea majira ya saa 8.55 leo mchana.

Wakielekea undani wa ajali hiyo baadhi ya mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio wakiwemo wafanyakazi wa Hoteli ya Kitonga walisema kuwa dereva wa Tax hiyo ambaye alikuwa na wenzake wawili katika gari hilo kabla ya ajali hiyo walikuwa wamesimama katika Hotel ya Kitonga kwa zaidi ya saa moja wakinywa pombe.

Hata hivyo baada ya kutoka katika Hoteli waliondoka huku wakiwa wamelewa hali iliyopelekea kushindwa kufunga hata buti la garil hilo na kuondoka bila kufunga alisema mmoja kati ya watumishi wa hoteli hiyo ambaye hata hivyo hakupenda kutaja jina lake.

Kwa upande wake majeruhi Ritha Masawe (30) mkazi wa Mbinga mkoani Ruvuma ambaye alikuwemo katika basi la Sumry alisema kuwa wakati ajali hiyo ikitokea yeye alikuwa siti yam bale jirani na dereva na kushuhudia jinsi ambavyo dereva huyo wa Salon alivyokuwa akiyumba katikati ya barabara .

Alisema eneo hilo ambayo lilna kona kali bado dereva huyo wa Salon akiwa katika mwendo mkali huku akiyumba kupita kiasi alilazimisha kulipita gari lenye namba za usajili T 633 AVF Pick Up Mitsubishi huku mbele basi hilo la Sumry likishuka mtelemko huu wa Kitonga.

“Kweli dereva huyo wa basi amefanya jitihada kubwa sana katika kulikwepa gari hilo dogo ambalo lilikuwa likija kama halina dereva ndani ….vinginevyo katika ajali hii kulikuwa hakuna mtu wakupona”

Kwa upande wake abiria Novatus Haule (29) mkazi wa Dar es Salaam ambaye alikuwa akitokea Songea alisema kuwa dereva wa basi hilo la Sumry kama angelikuwa katika mwendo mkali yawezekana vifo vya watu wengi zaidi vingeweza kutokea .

Hata hivyo alisema kama si dereva huyo kutumia mbinu kuwanusuru kwa kuligongesha basi hilo kwenye ukingo wa barabara kulikuwa na uwezekano wa basi hilo kutumbikia korongoni kabisa .

“kama unavyo ona mwenyewe Mwandishi hili basi likening’inia hewani … kama si hivyo tungezama bondeni huko”

Alisema kuwa chanzo cha abiri wawili waliokuwemo katika gari hiyo ndogo kufa ni kutokana na mwendo mkali ambao Tax hiyo ilikuwa nao kabla ya kuligonga basi hilo .

Haule alisema kuwa waliokufa katika ajali hiyo ni watu wawili pekee ambao wote walikuwa katika Tax hiyo wakitokea Dar es Salaam kuelekea Iringa.

Huku majeruhi watatu wa ajali hiyo wakikimbizwa katika hospitali teule ya wilaya ya Kilolo (Ilula) kwa matibabu zaidi .

Uongozi wa hospitali hiyo chini ya mganga mkuu Dr Mango umekili kupokea majeruhi watatu ambapo wawili akiwemo mzungu mmoja wametibiwa na kuruhusiwa huku majeruhi Juma Jabiri (34) mkazi wa Dar es Salaam ambaye ni dereva aliyekuwemo katika Tax hiyo hali yake ikiwa mbaya na hadi jana majira ya saa 10 jioni alikuwa akipumua kwa mashine maalum.

Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Claus Mwasyeba amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwa jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi zaidi.


Hata hivyo alisema watu hao wawili waliopoteza maisha katika ajali hiyo bado majina yao hayajafahamika japo wote ni wanaume watu wazima.

Imeandaliwa na Francis Godwin mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima Iringa

pata picha zaidi hapa

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA