Home » » BREAKINGNEWzzzzzzzzzz UMAGA AMEFARIKI DUNIA

BREAKINGNEWzzzzzzzzzz UMAGA AMEFARIKI DUNIA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, December 7, 2009 | 4:58 AMKwa mujibu wa taarifa zilizotua hivi punde katika mtandao huu zinadai kuwa Umaga ‘Eki Addie Fatu ‘mwenye miaka 36 alikuwa nyumbani kwake hajitambui na mkewe ambaye alimkimbiza hospitali amefariki dunia nyumbani kwake Houston kwa ugonjwa wa moyo ,ambako alipata tena mshtuko wa moyo kwa mara ya pilikabl/a ya kufariki dunia.


Mcheza mieleka huyo alikuwa akifahamika kwa michoro ya tattoo aliyokuwa akijichora pia anafahamika sana kwa sababu ya familia aliyotokea ambayo ni mashuhuri kwa mchezo wa mieleka,Fatu au Umaga umaarufu wake ulijitokeza zaidi mwaka 2007 alipofanya vizuri katika mashindano ya Wrestlemania na hivi karibuni Umaga alikuwa nchini Australia akitangaza mchezo wa mieleka.

Umaga anatokea familia ya Samoan ambayo inafahamika kwasababu ya kukuza biashara ya mchezo wamieleka na tangu enzi za mjomba wake ,kaka zake na sika Anojia ambao walifahamika kama The Wild Samoans katika miaka ya 1970 na 1980 pia yupo binamu yake aitwaye Dwayne ‘The Rock Johnson ‘ambaye aliacha mieleka na hivi sasa ni muigizaji wa Hollywood

Wengi wetu akiwemo kaka yangu Francis Tumbo tuataendelea kumkumbuka Umaga kwa jinsi ambavyo alivyokuwa akivutia katika michezo yake mbali mbali na pamoja na kumpenda na kumtamani kuendelea kuwa naye mwenyezi Mungu kampenda zaidi yetu hivyo hatuna budi kuendelea kumwombea heri ili Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi Amina
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA