Home » » BREAKINGNEWzzzzz MWALIMU NA FAMILIA YAKE HOI KWA KULA CHAKULA ,MWANAFUNZI ILALA AJINYONGA HADI KUFA

BREAKINGNEWzzzzz MWALIMU NA FAMILIA YAKE HOI KWA KULA CHAKULA ,MWANAFUNZI ILALA AJINYONGA HADI KUFA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, December 8, 2009 | 10:52 AMWatu watatu wakazi wa kijiji cha Pomelini wilaya ya Kilolo mkoani Iringa akiwemo mwalimu wa shule ya Msingi Pomelini Reah Nyawami wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa baada ya kula chakula kinachosadikika kuwa na sumu.

Wagonjwa hao ambao wamelazwa katika wodi namba 8 na 10 katika hospitali hiyo wanadaiwa kula ugali na mboga aina ya maharage ambapo kimoja wapo kinasadikika kuwa na sumu.

Akizungumza na mtandao huu hospitalini hapo leo mwalimu Mnyawami ambaye kwa sasa yeye amepata nafuu pamoja na jukuu wake Nanci Bavoni (6) alisema kuwa tukio hilo lilitokea dedsemba 7 majira ya mchana ambapo alipata kuandaa chakula na kula na familia yake hiyo.

"Kweli hadi sasa bado napata wakati mugumu kuweza kubaini sumu hii imetoka wapi katika chakula ....kwani unga uliotumika ni ule ambao nimekuwa nikitumia siku zote na zaidi ya mara 10 sasa nimekuwa nikipika ugali kwa kutumia unga huu pamoja na maharage haya haya ambavyo vyote nimelima mwenyewe na hata siku moja sijapata kuweka dawa kwa ajili ya kuzuia wadudu"

Anasema mwalimu huyo kuwa siku hiyo alitangulia kupika mboga na baada ya hapo alipika ugali huku mboga ikiwa jikoni na nyumba yake imezungushiwa uzio hivyo hakuna mtu ambaye alikuwa amepata kuingia kwa wakati huo.

Hata hivyo baada ya kumaliza kula chakula hicho cha mchana anadai kuwa alielekea bafuni kuoga na huko ndipo alipoanza kubaini dalili za kuishiwa nguvu na kuhisi kuwa yawezekana ni matatizo ya PB na hata alipojaribu kukanyaga chini alihisi kama anakanyaga hewani na ndipo alipojivuta hadi ndani na huko kukutana na mjukuu wake huyo akiwa ameishiwa nguvu.

Mbali ya mjukuu huyo pia mfanyakazi wake wa ndani Anjelo Magedenge (40) pia alikutwa akiwa hoi na ndipo wasamaria wema walipowakimbiza hospitali ya mkoa wa Iringa.

Mazingira ya sumu hiyo bado yanazua utata zaidi ambapo kaimu mnaga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Iringa Dr Ngala Mwalusamba amekili kupokea wagonjwa hao huku akidai hali ya mwalimu huyo na mtoto Nanci ni nzuri huku Anjelo akiendelea kupatiwa matibabu na akiwa bado kujitambua.

Wakati huo huo mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Ilala Jenelari Ngunda (4) amekufa baada ya kujinyonga katika mazingira tata na kuacha maswali mengi kuliko majibu.

Pamoja na baba mzazi wa mtoto huyo Victor Ngunda kudai kuwa mtoto huyo alikutwa akitokwa na povu mdomoni huku akiwa amejifunga kamba shingoni ,ila bado kamba yenyewe haikuweza kuonyesha wazi kama ingeweza kusababisha kifo cha mtoto huyo.

Alisema kuwa kamanda hiyo wakati kifo hicho kikimkuta mtoto huyo alimtuma mdogo wake kuchukua kibatari kwa ajili ya kutumia kupanga nguo ila baada ya kurudi ndipo aliposhuhudia kaka yake akiwa amejinyonga.

Baba wa mtoto huyo anasema kuwa baada ya kupata taarifa hiyo alijaribu kumfungua shuka hilo shingoni na kupiga simu polisi na baada ya polisi kufika kwa muda mwafaka ndipo walipomkimbiza hospitali ambapo wakiwa njiani mtoto huyo alifariki dunia.

Pamoja na kifo cha mtoto huyo pia mama mzazi wa mtoto huyo Bi Eliza Kalengela amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa baada ya kupoteza fahamu akiwa nje ya chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa Iringa jana mchana.
MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA