Home » » BODI YA MIKOPO YAWACHIMBA MKWARA WAHITIMU WA VYUO NCHINI

BODI YA MIKOPO YAWACHIMBA MKWARA WAHITIMU WA VYUO NCHINI

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, December 13, 2009 | 12:03 AM

MKURUGENZI wa urejeshaji wa mikopo wa bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HSLB)nchini Juma Hamis Changonja (pichani)amesema kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa wanafunzi wa elimu ya juu ambao wamesoma kwa mikopo na kushindwa kurejesha kwa wakati.
Mkurugenzi huyo alitoa kauli hiyo jana wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo kishiriki cha elimu Mkwawa (MUCE) mkoani ambapo wahitimu zaidi ya 800 waliweza kuhitimu katika chuo hicho katika fani mbali mbali ikiwemo ya elimu
Alisema kuwa lengo la serikali kutoa mikopo hiyo limelenga kuendelea kuboresha kiwango cha elimu nchini na kuwawezesha wanafunzi wengi zaidi ambao hawana uwezo kujisomesha kuweza kuendelea kunufaika na mikopo hiyo iwapo wakopaji watajenga utamaduni wa kurejesha kwa wakati.
Kwani alisema kuwa ili kuhakikisha mikopo hiyo inaendelea kuwanufaisha wanafunzi wengine waliojiunga na vyuo vikuu hapa nchini na wale wanaotaraji kujiunga mbele ya safari ni vizuri wote waliosoma kwa mikopo kuhakikisha wanarejesha mikopo hiyo kwa wakati ili iweze kukopeshwa kwa wengine na watakao shindwa kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria.
"katika kuhakikisha kuwa mikopo yote iliyotolewa kwa wanafunzi wa elimu ya juu wanairejesha kwa wakati ....bodi imeweka utaratibu wa kuwabana wale wote wanaoshindwa kurejesha mikopo hiyo baada ya kupata ajira" anasema mkurugenzi huyo
Kuwa upo utaratibu wa kuwabana watumishi wa serikali na wale wa sekta binafsi ambao wamesoma kwa mikopo ya serikali na iwapo itabainika kuwa wakopaji wanakwepa kusudi hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Chagonja alisema ili wahitimu hao wa chuo cha elimu Mkwawa ambao wengi wao wamesoma kwa mikopo hiyo kuepuka kufikishwa mahakamani kwa kushindwa kurejesha mikopo ni vyema pindi watakapo pata ajira kuanza kurejesha mikopo hiyo taratibu hadi watakapo maliza madeni yao yote.
Hata hivyo alisema kuwa bodi ya mikopo inayo majina ya watu wote ambao wamesoma kwa mikopo na kuwa iwapo wataendelea kusua sua katika urejeshaji watawajibishwa kisheria.
MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA