Home » » BEYOND SKY YATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI 14 KWA AJILI YA UJENZI WA SHULE ...........

BEYOND SKY YATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI 14 KWA AJILI YA UJENZI WA SHULE ...........

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, December 18, 2009 | 5:01 AM


Mkurugenzi wa Beyond Sky (kulia) akiwa ameshika tango lenye kiwango cha fedha ambazo kampuni yake imechangia kijiji cha Mangawe kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingiAkikabidhi msaada wa fedha hizo taslim kwa kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Joseph Mbiaji katika hafla fupi iliyofanyika kijiji hapo jana , mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Beyond Sky Kritsana Massepha alisema kuwa pamoja na kuwa bado kampuni hiyo ipo katika utafiti wa awali kwa ajili ya uchimbaji wa kopa katika kijiji hicho ila imegushwa na adha kubwa wanayoipata wanafunzi wanaosoma elimu ya msingi katika kijiji hicho cha utafiti ambao wamekuwa wakitembea mwendo mrefu kufuata elimu.


Alisema kuwa toka shule ya msingi ilipo na kitongoji hicho ni mwendo wa masaaa mawili na zaidi hivyo kwa wanafunzi kutembea kwa mwendo huo kwenda kufuata elimu ni kazi kubwa hali iliyopelekea kampuni yake kugushwa na kuamua kuchangia kiasi hicho cha shilingi milioni 14 kwa awamu ya kwanza kwa ajili ya kuhamaisha ujenzi wa shule ya msingi mkondo 'B'

Hata hivyo alisema kuwa kampuni hiyo itaendelea kuchangia ujenzi huo hadi utakapokamilika na kuwa lengo likiwa ni kuboresha ubora wa elimu kwa watoto wa eneo hilo.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa kabla ya kuamua kuchangia ujenzi huo mbunge wa jimbo la Ismani na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam William Lukuvi alifika ofisini kwake na kumwomba msaada huo kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa shule hiyo .

Pamoja na kuchangia ujenzi huo pia alisema kuwa bado kampuni hiyo ambayo imekusudia kujenga kiwanda cha uchimbaji kopa katika kijiji hicho itaendelea kuchangia shughuli za kimaendeleo katika kijiji na kata hiyo ili kuwawezesha wananchi wake kupiga hatua zaidi ya kimaendeleo.

Hivyo alisema katika kuhakikisha maendeleo yanakuwepo uongozi wa kampuni hiyo utakutana na wananchi pamoja na viongozi wa kijiji hicho ili kujua mahitaji yao ya msingi kabla ya kampuni yake kuchangia.

Kwa upande wake katibu wa mbunge wa jimbo la Ismani Thom Malenga akishukuru kwa niaba ya mbunge Lukuvi alisema kuwa mkurugenzi huyo wa Beyond Sky ameonyesha mfano mwema kwa makampuni mengine hapa nchini kwani pamoja na kuwa bado hata kujua kiwango cha madini yaliyopo kampuni hiyo imeanza kutoa fedha zake mfukoni kusaidia maendeleo ya wananchi.

Malenga alisema kuwa moja ya kero kubwa kwa wananchi wa kitongoji hicho ni elimu ya msingi ambayo watoto wao wamekuwa wakiipata kwa kutembea kwa mwendo mrefu zaidi ukilinganisha na vijiji vingine.

Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Iringa Mbiaji alisema kuwa halmashauri yake inathamini mchango mkubwa uliotolewa na kampuni hiyo na kuwataka wananchi wa kijiji hicho kutoa ushirikiano mkubwa pale wanapotakiwa kufanya kazi katika kampuni hiyo.

Kwani alisema kuanzishwa kwa kampuni hiyo mbali ya kuliingizia Taifa kipato pia wananchi wenye sifa za kufanya kazi watanufaika na kampuni hiyo .
MWISHO

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA