Home » » TRA IRINGA YAWAKWAZA WANAMICHEZO .......

TRA IRINGA YAWAKWAZA WANAMICHEZO .......

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Wednesday, November 25, 2009 | 5:49 AM


MCHEZO wa ufunguzi wa wiki ya mlipa kodi kati ya mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa na wafanyabiashara wa manispaa ya Iringa uliochezwa jana umeingia dosari baada ya wachezaji wa timu ya wafanyabiashara kuficha mpira wa TRA kama njia ya kulipiza kisasi kwa uongozi wa TRA Iringa kushindwa kutoa zawadi iliyotangazwa kwa mshindi na badala yake kutoa kuku wa shilingi 1500 .

Pamoja na kutoa zawadi ambavyo iliwafanya wachezaji wa timu hiyo ya wafanyabiashara kuanzisha zogo na baadhi yao wakiutaka uongozi wa timu hiyo kususia kupokea zawadi hiyo ya mtoto wa kuku ,pia aliyekuwa mgeni rasimi katika mchezo huo mkuu wa wilaya ya Iringa Aseri Msangi aliyewakilishwa na katibu tarafa wa Manispaa ya Iringa Twaha Kimbama alilazimika kuongeza fedha yake mfukoni kiasi cha shilingi 10,000 ili kuwapoza waamuzi hao wanne ambao awali ni bajeti ilitengwa ya watatu pekee.

Kwa mujibu wa matangazo ya TRA yaliyokuwa yakitaganzwa katika gari la matangazo kwa ajili ya kuhamasisha wadau wamichezo kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo uliokuwa katika uwanja wa Samora yalionyesha kuwa mshindi wa mchezo huo angejinyakulia zawadi nono iliyokuwa imeandaliwa na TRA mkoa wa Iringa.

Hata hivyo matumaini ya zawadi hiyo yalionekana kupotea baada ya timu ya wafanyabiashara Manisapaa ya Iringa kufanikiwa kutoa kichapo cha magoli 2-0 dhidi ya vigogo hao wa TRA .

Wakizungumuzia zawadi hiyo wachezaji wa timu ya wafanyabiashara walisema kuwa hawakutegemea kama kungekuwa na zawadi ndogo kiasi hicho na kuwa awali kiongozi wao Omary Abdalah aliwaeleza kuwa mshindi wa mchezo huo ameandaliwa zawadi nono isiyopungua shilingi 200,000 ila matokeo yake wameambulia kuku ambayo hata shilingi 4000 vigumu kuuzwa.

Hivyo walisema kuwa hawatakuwa tayari kucheza mchezo wa wowote na TRA iwapo zawadi hazitaonyeshwa mapema kwa uongozi wa chama cha soka manispaa ya Iringa kama .

Kwani walisema kitendo kilichofanywa na uongozi wa TRA mkoa wa Iringa ni sawa na kuwakatisha tamaa vijana wapenda soka ndani ya mkoa wa Iringa ambao wamekuwa wakitambua kuwa soka ni moja kati ya ajira kwa wanamichezo.

Pia walisema kuwa TRA mkoa wa Iringa imekuwa ikijigamba kuwa imekusanya mapato zaidi ya malengo huku ikionyesha kufanya ufisadi wa wazi kwa wana michezo kwa kugeuza zawadi ya mshindi na kuwa yawezekana kama timu ya TRA ingechukua ubingwa katika mchezo huo zawadi ambayo wangejizawadia ingekuwa ni mamilioni ya shilingi .

Kwa upande wake kocha wa timu ya wafanyabiashara Omary Abdalah alisema kuwa mbali ya kujipongeza kwa ushindi huo ila bado zawadi waliyopewa imeonyesha kuwakatisha tamaa wachezaji na kuna uwezekano wa wachezaji hao kutokuwa tayari kucheza na TRA wakati wakilele cha maadhimisho ya wiki ya mlipa kodi kama walivyoomba .

Alisema kuwa kuku ambaye walipewa zawadi kama washindi wamelazimika kuiuza kwa mmoja kati ya wachezaji kwa kiasi cha shilingi 1500 pekee baada ya wateja kugoma kununua kwa shilingi 3000.

Wakielezea kuhusiana na zawadi hiyo baadhi ya wanachama wa chama cha waandishi wa habari zamichezo Tanzania (TASWA) mkoa wa Iringa walisema kuwa ni vema kwa wakati mwingine timu zisikubali kuingia kushiriki mashindano bila kujua taratibu zaushiriki ili kuondoa lawama zinazoepukika.

TASWA imesema kuwa TRA ilikuwa na uwezo wa kuandaa hata ngao inayoelezea wiki ya mlipa kodi na umuhimu wakulipa kudi kama sehemu ya zawadi kwa mshindi badala ya kutoa zawadi ya kuku ambayo kimsingi haihamasishi michezo bali inarudisha nyuma jitihada za vijana kupenda michezo.

Habari hii imeandaliwa na Francis Godwin mwenyekiti wa TASWA mkoa wa Iringa na mwandishi wa gazeti la Tanzania daima
MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA