Home » » TASWA IRINGA KESHO KUADHIMISHA SIKU YA UKIMWI NA YATIMA

TASWA IRINGA KESHO KUADHIMISHA SIKU YA UKIMWI NA YATIMA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, November 30, 2009 | 4:20 AM

CHAMA cha waandishi wahabari za michezo Tanzania (TASWA) mkoa wa Iringa (Desemba mosi) kuadhimisha siku ya UKIMWI duniani kwa mchezo wa kirafiki wa hisani kati yake na watoto yatima pamoja na watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI .

Katika mchezo huo ambao mwandishi wa habari za gazeti hili mkoani Iringa Francis Godwin ambaye ni mwenyekiti wa muda wa TASWA Iringa amejitolea kiasi cha shilingi 150,000 kwa ajili ya zawadi kwa washindi ,TASWA Iringa imewaomba wadau wengine kujitokeza kuchangia watoto hao yatima kama sehemu ya kuadhimisha siku ya UKIMWI duniani ambayo kimkoa inafanyika wilaya ya Mufindi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana juu ya mchezo huo makamu mwenyekiti wa TASWA Iringa Rashid Msigwa alisema kuwa mchezo huo utachezwa katika uwanja wa Samora kuanzia majira ya saa 10 jioni na kuwataka wapenzi wa soka na wadau wa maendeleo mkoa wa Iringa kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo.

Msigwa alisema kuwa maandalizi yote kwa ajili ya mchezo huo yamekamilika na kumpongeza Godwin kwa kutoa wazo hilo la kuwa na mchezo wa hisani kwa ajili ya kuadhimisha siku ya UKIMWI .

Alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa zawadi kwa mshindi wa kwanza na wapili ila bado kama timu ya waandishi wa habari itashinda zawadi zote zitarejeshwa kwa timu ya Yatima na watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI kama sehemu ya kuwakumbuka .

Hata hivyo alisema awali TASWA ili kuwa imepanga kila mwanahabari ambaye angeshiriki mchezo huo angepaswa kuchangia kiasi cha shilingi 2000 kama sehemu ya usajili wake fedha ambazo zingetumika kutunisha michango ya mchezo huo kwa ajili ya yatima ila fedha hizo hazijatolewa na badala yake wachezaji wataungana na watazamaji wengine kuchangia baada ya mchezo huo.

Pia alisema katika mchezo huo hakutakuwa na kiingilio chochote ila mashabiki wanakumbushwa kutembea na michango yao kwa ajili ya watoto hao.

Alisema kuwa TASWA itacheza na timu ya yatima na watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI kutoka kata ya Ilala mjini Iringa na diwani wakata hiyo Grevas Ndaki ndiye atakuwa mgeni rasimi katika mchezo huo.

MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA