Home » » SIRI NZITO YAFICHUKA MAUWAJI YA WANAFUNZI VETA IRINGA

SIRI NZITO YAFICHUKA MAUWAJI YA WANAFUNZI VETA IRINGA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, November 13, 2009 | 11:03 PM


SIRI zito yafichuka juu ya vifo vya wanafunzi wa kike wawili katika chuo cha ufundi stadi (VETA) Iringa waliouwawa kwa kupigwa na risasi na mmoja kujeruhiwa na kijana ambaye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mmoja kati ya wanafunzi hao ,ungana na mwanahakati wa kweli Francis Godwin katika ufuatiliaji wa kisa hiki.

Kabla ya kuuwawa waliingizwa chini ya daraja la kulazwa kifudi fudi na kucharazwa fimbo kila mmoja kabla ya muuaji huyo kuwapora simu zao za viganjani na kuwataka kusali sara zao za mwisho kwa madai kuwa amechoka na tabia ya mpenzi wake kuendelea kumkataa kila wakati na hivyo ameamua kuwaua wote watatu .

Pia gari aina ya saloon lenye namba T118AH Toyota Mark II ambalo lilitumiwa na muuwaji huyo kuwateka mabinti hao hadi kijiji cha Kitayawa wilaya ya Iringa vijijini umbali wa km zaidi ya 150 kutoka Iringa mjini dereva wake alikuwa ni deiwaka na aliazimwa gari hilo kwa muda na mmiliki wake aliyefahamika kwa jina moja la Nico kutoka mjini Njombe na ndipo walipotoroka na muuwaji huyo hadi mjini Iringa kuja kufanya unyama huo.

Akielezea juu ya mazingira ya kifo cha wanafunzi hao mzee Mustaphar Sapi Mkwawa ambaye ni babu wa marehemu Rehema Ismail (24) ambaye ndiye alikuwa mwenyeji wa wenzake hao wawili waliokuwa wakiishi chumba kimoja katika nyumba ya mzee huyo eneo la Mshindo mjini Iringa wakati wakiwa masomoni.

Alisema kuwa mjukuu wake huyo wazazi wake wapo mkoani Dodoma kikazi na alifika mkoani Iringa miaka miwili iliyopita kwa ajili ya kuja kuanza masomo katika chuo hicho cha Veta na wakati wote alikuwa akiishi chuoni na baada ya kuanza mwaka tatu ndipo walipohama chuoni na kuamua kuishi nyumbani pamoja na wenzake hao ambao aliwakaribisha.

Aliwataja wenzake hao kuwa ni Labda Pampema (23) mkazi wa Kibondo na Cotrida Luvingo ambaye ni mkazi wa Ndiwili wilaya ya Iringa vijijini ambao wote walikuwa wamepewa hifadhi na mareheme Rehema eneo hilo la Msindo.

Mzee Mkwawa alisema kuwa siku zote wanafunzi hao walikuwa ni marafiki wa karibu na hata siku ya tukio ambayo ni Novemba 5 majira ya saa 11 asubuhi walirejea wote watatu kutoka katika msiba wa mzee Wiliam Chaula ambako walikuwa wamelala na baada ya kufika nyumbani hapo umbali wa mita kama 200 hivi kutoka msibani waliigonga mlango na kuingia ndani na wakati huo Tax ya muuwaji huyo ilikuwa ikiwasubiri nje .

"Mimi wakati huo nilikuwa nimelala ila nilipochungulia nje niliona Tax hiyo ambayo ilikuwa ikiwasubiri wajukuu wangu ....baada ya hapo waliondoka huku kukiwa na malumbano ya hapa na pale lakini kubwa nilisikia kuwa wanakwenda kuchukua zawadi "

Alisema mzee huyo kuwa muuwaji huyo ambaye hata hivyo hatambuliki kabisa katika familia yao kuwa aliwadanganya wanafunzi hao kuwa yeye anataraji kuhamia mjini Iringa kutoka Njombe hivyo kuna mizigo ambayo anataka kuwaagiza ili waje waihifadhi mjini Iringa,mizigo ambayo kwa wakati huo alidai kuwa ipo Ipogolo .


Hata hivyo baada ya kuwadanganya mabinti hao hadi Ipogolo bado alipofika eneo husika ambalo ni Ipogolo aliendelea na safari kwa kubadili kauli nyingine tena kuwa anataka kufika hadi kijiji cha Ndiwili wilaya ya Iringa vijijini umbali wa kilimota zaidi ya 20 kutoka Ipogolo kwa madai kuwa anataka kufika hadi nyumbani kwa wazazi wa mpenzi wake huyo Cotrida Luvingo (22) ili kwenda kuwasalimia na kujitambulisha rasmi pamoja na kukataliwa kimapenzi na binti huyo.

Mzee huyo alisema kwa maelezo ya majeruhi wa tukio hilo Cotrida Luvingo alisema kuwa hata walipofika kijijini kwao bado gari liliendelea na safari jambo ambalo liliwafanya kupatwa na wasiwasi na wote watatu kupigwa na bumbuwazi na kukaa kimya bila kuzungumza chochote kutokana na kuingia na hofu na jinsi ambavyo muuwaji huyo alivyoanza kubadilika sura yake pamoja na mazungumzo kwa kutoa vitisho na misamiati miti juu yao.

Alisema walipofika eneo la kijiji cha Kitayawa gari lilisimama kando ya daraja la ghafla muuwaji huyo Bw Leopard Mkolwe (23) na dereva wake walishuka katika Tax na kusimama nje kwa sekunde chache kisha kufungua milango ya gari hilo na kuwataka wote kushuka ndani ya gari huku wakiwaonyesha bastola na kuwaeleza kuwa kuanzia saa hiyo wapo chini ya ulinzi na hahawatakiwi kujfanya chochote zaidi ya kutii kile wanachoelekezwa.

"Anasema baada ya hapo waliingizwa chini ya daraja na kuamuliwa kulala kifudi fudi kwa madai kuwa waapaswa kuuwawa kujanzia sasa ...ila kabla ya kuwaua walikata fimbo na kuwacharaza sana wote watatu na baada ya hapo Cotrida alihoji sababu ya kuwaua wenzake hao ambao hqawahusiki kwa chochote katika mapenzi hayo na hivyo kutaka auwawe yeye na sio rafiki zake hao wawili...."

Alisema pamoja na ushauri huyo wa mpenzi wake bado muuwaji huyo alionyesha msimamo wake huku akidai kuwa lazima wote wapotee kwa madai kuwaacha hai wenzake hao ni kujitengenezea ushahidi na watakwenda kutoa siri ya tukio hilo.

Hapo ndipo alipoanza kumpiga risasi mpenzi wake Cotrida japo kutokana na haraka ya muuwaji huyo hakuweza kumlinga vizuri zaidi ya risasi hiyo kumkwaruza kidogo sehemu ya shavu lake na kutokana na damu kutoka kwa wingi na mpenzi wake huyo kupoteza fahamu kwa muda na wenzake kupigwa katika paji la uso wote aliamia kuwa wote wamekufa na hivyo kuingia katika gari lao na kukimbia eneo hilo huku maiti hizi zikitelekezwa chini ya daraja.

Mkazi wa kijiji cha Kitayawa ambaye alipata kushuhudia mauwaji hayo Kefa Sangawe alisema kuwa toka eneo la tukio la alipokuwepo yeye akiendelea na shughuli zake za shamba ni kama mita 210 hivi na kuwa kwa kiasi aliweza kushuhudia tukio hilo.

Pamoja na kushuhudia mabinti hao wakishushwa katika gari na muuwaji huyo na dereva wake bado alishindwa kusogea jirani baada ya kuona bastola ,ila baada ya muuwaji huyo na mewenzake kukimbia eneo hilo aliweza kupiga kelele na wananchi kufika eneo hilo kutoa msaada kwa Cotrida ambaye alikuwa mzima .

"Mimi mkononi nilikuwa na jembe na panga mwanzoni nilijua wanawake hao na huyo jamaa na mwenzake wanashuka chini ya daraja kwa ajili ya kwenda kufanya mapenzi ama kujisaidia ila baada ya kusikia vilio kutoka kwa mabinti hao nikajua wazi kuwa kuna shari huko ...baada ya muda nikasikia milio ya risasi iliyofuatana mara tatu kweli kwa hofu mkojo ulianza kunitoka na mimi kupatwa na bumbuwazi kuwa yawezekana baada ya kuwaua hao itafuata zamu yangu....yule jamaa njinsi alivyovaa mabuti yake ukimwona hana tofauti na komandoo"

Mkuu wa chuo cha Veta Iringa Alhonce Lubasha alisema kuwa wanafunzi hao ambao walikuwa mwaka wa tatu wakisomea masomo ya udhamili na Kompyuta walikuwa ni miongoni mwa wanafunzi bora katika chuo hicho katika masomo.

Hata hivyo alisema tabia za wanafunzi hao chuoni hapo zilikuwa ni nzuri na hata siku moja chuo hakijawahi kupokea malalamiko wala kutoa adhabu yoyote kwao kwa utovu wa nidhamu kama ilivyo kwa wengine.

"Sisi kama chuo kweli kifo cha wanafunzi hao tumepokea kwa masikitiko makubwa na kwani kati ya wanafunzi ambao tulikuwa tukiwategemea hapa chuoni ni pamoja na wanafunzi hao ...nasema hata tulipokea taarifa juu ya vifo hivyo walimu na wanafunzi kweli tul,ichanganyikiwa sana"

Hata hivyo alisema kuwa mwanafunzi Cotrida Luvingo pamoja na kusoma Veta pia alikuwa ni karani katika chuo kikuu kishiriki cha Ruaha (RUCO) mkoani Iringa.

Akielezea jinsi walivyo aga katika msiba muda mchache kabla ya kifo chao Grace Chaula alisema kuwa mabinti hao walikuwa wamelala pamoja msibani na asubuhi waliaga kuwa wanakwenda kujiandaa kwa ajili ya kwenda shule .

"Hawa mabinti tulikuwa nao katika msiba usiku wote na wote walilala msibani na asubuhi waliondoka kwa madai wanawenda kujiandaa kwa ajili ya shule ....hivyo niliposikia wameuwawa kweli sikuamini kabisa "

Baadhi ya wanafunzi na watumishi wa chuo cha Veta wameeleza kusikitishwa na vifo vya wanafunzi hao na kuwa siku moja kabla wanafunzi hao waliouwawa walikuwa ni watu wenye mawazo mengi tofauti na siku nyingine ambazo walikuwa ni wacheshi kupita kiasi na ni watu wasio penda makuu.
Pia walisema vifo hivyo ni fundisho kwa wanafunzi wengine na wanawake mkoani Iringa kuepuka kuwa na mahusiano na vijana wasio eleweka na kupenda zawadi visizo za jasho lao .
Mmoja kati ya madereva Tax wilaya ya Njombe alimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na mazoea ya kumkodi deiwaka huyo kila wakati na kuwa hivyo yawezekana kabisa mipango ya mauwaji hao ilipangwa wote.

Hata hivyo alihoji umiliki wa bastola hiyo aina ya Browing yenye namba A6892 ambayo ilitumika kufanya mauwaji hayo ,kuwa yawezekana kabisa muuwaji huyo amekuwa akimiliki bastola hiyo kinyume na kufanya ujambazi katika maeneo mengi mkoani Iringa.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na uwazi umebaini kuwa kijana huyo muuwaji Bw Peopard alikuwa akilelewa na Paroko wa kanisa la Romani Catoriki Parokia ya Ihanga wilaya ya Njombe aliyefahamika kwa jina la Wido na hivyo baada ya kufukuzwa na Paroko huyo kutokana na tabia yake mbaya ikiwemo ya udokozi ndipo alipopora bastola hiyo.

Pamoja na Paroko huyo kuibiwa bastola hiyo ila hajapata kutoa taarifa katika vyombo vya usalama hali inayotiliwa shaka na wengi mkoani hapa na kutaka jeshi la polisi mkoa wa Iringa kumkamata Paroko huyo na kumuunganisha katika kesi hiyo ya mauwaji hasa kwa hatua yake ya kushindwa kutunza silaha yake na wala kutoa taarifa pale ilipoibiwa .

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Bw,Evarist Mangalla alielezea mazingira ya kukamawa kwa matuhumiwa hao wa mauwaji kuwa ni pamoja na ushirikiano wa wananchi kupitia dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi .

Kwani alisema kuwa baada ya kufanya mauwaji hao watuhumiwa hao walifanikiwa kupita wilaya ya Iringa vijijini,wilaya ya Mufindi na baada ya kufika kizuizi cha wilaya ya Njombe (check Point ) Makambako ndipo walipokamatwa na polisi huku wakiwa na bastola hiyo iliyotumika katika mauwaji .

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo Bw Mkolwe ambaye ni mkulima na mkazi wa kijiji cha Ihanga wilaya ya Njombe pamoja na dereva wake Emily Ngailo (23) mkazi wa mji wa Njombe walikuwa na bastola hiyo na wote walikamatwa na kufikishwa mahakamani juzi.

Hata hivyo watuhumiwa hao ambao walifikishwa mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Iringa Self Kulita huku umati mkubwa wa wakazi wa mkoa wa Iringa ukijitokeza kwa wingi mahakamani hao ,walikana shitaka hilo na mauwaji na kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tena Novemba 19 mwaka huu.
MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA