Home » »

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, November 9, 2009 | 3:50 PM

Na Francis Godwin,Iringa

VILIO vya wakazi wa Manispaa ya Iringa jana vilisikika baada ya watu watano wanasadikika kufa na wengine saba kujeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospotali ya mkoa wa Iringa baada ya lori lenye namba za usajili T 789 AFN Fuso kuacha njia ya kugonga nyumba .

Huku waokoaji wakitumia mikoano kufukua kifusi ili kutoa maiti zilizokuwa zimefukiwa na kifusi hicho.

Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 9 Alhasiri katika eneo la Kihesa Sokoni Manispaa ya Iringa baada ya lori hilo ambalo lilikuwa bovu kufeli breck zake na kuparamia nyumba hiyo iliyokuwa upande wa kushoto mwa barabara kuu ya Dodoma –Iringa.

Wakielezea juu ya tukio hilo mashuhuda wa ajali hiyo walisema kuwa lori hilo lilikuwa kwa kitambo lilikuwa limeegeshwa mwishoni mwa mlima wa kuelekea Mtwivila mjini Iringa baada ya kuwa na matatizo ya klachi na gia.

Hata hivyo walisema kwa muda mmiliki wa lori hilo na dereva wake walikuwa wakilitengeneza lori hilo ambalo lilikuwa limeshehena magunia ya mkaa ,ila baada ya mmiliki wa gari hilo kutoka na kwenda mjini kufuata vifaa hivyo dereva aliliondoa lori hilo huku likiwa bovu.

Walisema Bw Juma Sanga na Kefa Kyando kuwa baada ya dereva kuondoa gari hilo na kuanza kushuka mteremko huo wa Mtwivila ghafla breck zilifeli na kupelekea lori hilo kuigonga nyumba hiyo ambayo nje kulikuwa na mafundi chelehani na vijana waliokuwa wakifanyabiashara ndogo ndogo.

Hata hivyo alisema kuwa sehemu kubwa waliokufa katika tukio hilo na wale waliokimbilia ndani ya nyumba hiyo wakati lori hilo likija kwa kasi .

“Hadi sasa ni miili ya watu wawili pekee imetolewa wote wakiwa wanawake …ila hapa nje walikuwepo watu zaidi ya watano ambao hawaonekani na kuna uwezekano wamefukiwa na kifusi “

Majeruhi wa ajali hiyo Deo Macha (40) alisema kuwa kwa upande wake alikuwa akipita barabarani na ghafla aliona lori hilo likishuka kama vile limepoteza mwelekeo na alipojaribu kukimbia bado liliweza kumfuata na kumgonga .

“Mimi nilikuwa napita njia na ghafla niliona lori hilo likija kama halina dereva huku honi zikipigwa mfululizo ….nilijaribu kukimbia ila bodi lilinigonga na kuanguka chini”

Akielezea juu ya vifo vya watu hao diwani wa kata ya Kihesa Mussa Wanguvu alisema kuwa msiba huu ni pigo kubwa kwa wakazi wa Manispaa ya Iringa ,kwani alisema mazingira ya ajali hiyo yanashangaza sana .

Kweli hapa nilipo nimepigwa na bumbuwazi baada ya kusikia tukio hilo mimi na madiwani wenzangu tulikuja haraka hapa ili kusaidia kuokoa majeruhi na kutoa maiti zilizokuwa zimefukiwa na kifusi ikiwa ni pamoja na kuomba msaada wa kuvuta lori ambalo lilikuwa limeingia ndani ya nyumba hiyo.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia umati mkubwa wa wananchi wa Manispaa ya Iringa na baadhi ya wasafiri wa mabasi ya Dodoma na Mtera wakiwa wamekwama safari zao kwa muda kwa ajili ya kusaidia kuokoa majeruhi hao wakisaidiana na viongozi wa serikali chini ya mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Terresia Mmbando na wale wa jeshi la polisi wakiongozwa na kaimu kamanda huyo.

Hata hivyo jitihada za vibaka kupora mali za marehemu hao zikiwemo cherehani na magodoro ziligonga mwamba baada ya askari polisi na wananchi kufanikiwa kukamata vitu hivyo ambavyo vibaka walikuwa wakitaka kukimbia navyo.

Pamoja na vibaka hao kuthibitiwa bado sehemu kubwa ya wananchi walikuwa wameshika vichwa huku kila mmoja akilia kwa uchungu kutoka na vifo vya watu hao .

Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Claus Mwasyeba alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwa bado jitihada za uokoaji zilikuwa zikiendelea hadi majira ya saa 10 jioni .

Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Iringa Dr Oscar Gabone alisema kuwa hadi saa 11 jioni maiti mbili zilikuwa zimefikishwa katika chumba cha maiti hospitalini hapo huku zikiwa zimeharibika kupita kiasi .

Pamoja na maiti hizo pia majeruhi saba walikuwa wamefikishwa na wengine wakiendelea kufikishwa hospitalini hapo.

Aliwataja majeruhi waliokuwa wamefikishwa hospitali hapo kuwa ni Deo Maucha (40) Adam Kapera,Haruna Ally(27),Seleman Lukinga(41) ,Selvesta Michael,Fotnatus Maro (37) Elina Mahuvi (20) na dereva wa lori hilo Edward Mwandele(47)Wakati maiti zilizofikishwa zilikuwa ni nne na kuzitaja maiti hizo kuwa ni ya Kelvin,Recho Mtonyole,EdsonMkulu na binti mmoja ambaye jina lake lilikuwa bado kutambuliwa .


Hata hivyo mtandao huu ulishuhudia majira ya saa 2.15 usiku majeruhi
Wakati majeruhi Suleiman Lukingo (41)mkazi wa Lugalo mjini Iringa akifariki dunia katika chumba cha wagonjwa mahututi ambako alikuwa amelazwa na kufanya jumala ya watu waliopoteza maisha katika tukio hilo kufikia watano huku jitihada za kutafuta miili ya watu wengine zikiendelea kufanywa hadi saa mbili usiku.

Taarifa zaidi juu ya tukio hilo utaipata katika mtandao huu ama katika gazeti la Amani siku ya Alhamisi kwa sasa tuzidi kuwaombea marehemu wote mapumziko mema mbinguni na afya njema majeruhi wa ajali hii.

MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA