Home » » KIFO CHA MWANAHABARI CHAZUA NGUNZO IRINGA ...............

KIFO CHA MWANAHABARI CHAZUA NGUNZO IRINGA ...............

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, November 3, 2009 | 10:06 AMMTAMBUE mwanahabari maarufu mkoa wa Iringa Rose Majani (pichani)aliyefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha na kifo chake kuzua utata mkubwa mkoani Iringa kutokana na kujiunga na dini inayozuia waumini wake kunywa dawa wala kwenda hospitali pale wanapoumwa bila ridhaa ya viongozi wa dini hiyo Mwandishi wetu FRANCIS GODWIN anaelezea zaidi katika safu hii ya mikasa ya maisha.

Yawezekana umepata kusikia mwenyewe ama kusimuliwa na ukaamini lah ukashindwa kuamini ila kwangu mimi nimepata kushuhudia na kusimuliwa na marehemu mwenyewe kabla ya kifo chake juu ya imani ya dini hii ambayo kwangu mimi naweza kuifananisha imani hiyo na imani potofu zinazopigwa vita na serikali zikiwemo zile za waganga wa kienyeji wanaoendelea kuliteketeza Taifa lisilo na hatia kwa hawa ndugu zetu na watanzania wenzetu watu wenye ulemavu wa ngozi (maalbino)kwa imani zao za kishirikina.

Ikumbukwe kuwa imeandikwa kuwa siku za mwisho kutakuwepo manabii wa uongo wengi sana na ili kukabiliana ni vyema kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kutulia katika dhehebu lako kwani kutanga tanga na madhehebu kuna faida na hasara zake na kama mwanahabari mwenzangu ndugu yangu mpendwa Rose Majani yawezekana kifo kisingemkuta ama kingemkuta ila sio kwa mazingira haya ya leo.

Kwa wakazi wa mkoa wa Iringa na watanzania wapenzi na Radio wapo FM ambayo pia ni moja kati ya vyombo vya habari ndugu na gazeti hili ,kifo cha mwanahabari huyo na utata uliogubika msiba huo kwao sio mgeni na leo nafanya kuwakumbusha kile kilichotokea.
Rose Majani kabla ya kujiunga na kanisa hilo ambalo jina lake kwa sasa limehifadhiwa kutokana na hatua za kiusalama zinazotaraji kuchukuliwa na serikali ya mkoa wa Iringa,alikuwa ni mwenye afya njema ambapo kwa wakati huo yeye na familia yake alikuwa akiabudu katika Kanisa la Roman Catoriki (RC) Parokia ya Mshindo mjini Iringa .

Ila baada ya muda Rose aliweza kujiunga na Kanisa hilo ambalo lilianzishwa mjini Iringa kwa kipindi cha miaka miwili hii likiwa na waumini wasio zidi 10 hivi ila kutokana na mbinu iliyotumiwa kwa kuwavuta baadhi ya watu wenye uwezo kanisa hilo liliweza kupata umaarufu mkubwa hadi kujulikana kwa kila mmoja na kupelekea mwanahabari huyo kujiunga .

Hata hivyo Mwanahabari huyo baada ya kujiunga hali yake kiafya ilianza kuyumba na hata kazini kwake Radio Country FM kwenda kwa shida hali iliyopelekea wafanyakazi wenzake kulazimika kwenda kumjulia hali kila wakati nyumbani kwake Mlandege mjini hapa huku wakati mwingine wakishindwa kumwona baada ya waamini wenzake kuwa katika maombi kama sehemu ya tiba kwa ugonjwa uliokuwa ukimsumbua .

Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa Abed Kiponza ambaye pia ni mwenyekiti wa Sumatra mkoa wa Iringa anasema kuwa siku moja kabla ya kifo cha mwandishi huyo Octoba 13 mwaka huu alifika nyumbani na kumkuta mgonjwa huyo akiwa katika hali mbaya na kuweza kufanya mahojiano mafupi kuhusiana sababu za kushindwa kwenda hospitali .

Kiponza anasema kuwa kwa kinywa chake mgonjwa huyo alipata kueleza sababu ya kutokwenda hospitali kwa madai kuwa dini yake hiyo hairuhusu kunywa dawa hivyo kwake isingekuwa rahisi kwenda kutibiwa kwa kuhofia kutengwa na waamini wenzake.

Hata hivyo mwenyekiti huyo anasema wao kama chama na serikali hawatakubali kuona watanzania wanaendelea kufa kwa imani potofu kama hizo na kuwa anafanya mawasiliano na mkuu wa mkoa wa Iringa ili viongozi wa dhehebu hilo kufukuzwa ndani ya mkoa wa Iringa.

Clement Sanga ,Oliva Moto , Denis Mlowe ,Zamoyoni Ngede na Rashid Msigwa ni baadhi ya waandishi wa habari wa Radio Country Fm Iringa ambayo ndiyo mwandishi huyo Rose Majani enzi wa uhai wake alikuwa akifanya kazi hapo ,wanasema kuwa kifo cha mwandishi huyo ni pingo kuwa kwa familia yake na ni pigo lisilozibika katika taalum hii ya habari.

Wanahabari hao wanasema Rose Majani ambaye enzi wa uhai wake alikuwa ni mtulivu na mcheshi kifo chake kwa asilimia 100 kimetokana na imani yake dhidi ya dini hiyo.

Kwa upande wake meneja wa Radio Country Fm Neema Kindole anasema kuwa kifo cha mwanahabari hiyo kwa kituo hicho cha Radio kimepokelewa kwa manjozi mengi kutokana na jinsi ambavyo marehemu huyo enzi za uhai wake alivyoweza kujituma katika kazi na kuwa mshauri mwema kwa wenzake.

Kindole anasema kama njia ya kumuenzi kituo hicho kwa siku tatu mfululizo kilisimamisha matangazo yake na kupiga nyimbo za maombolezo ,ikiwa ni pamoja na kugharamia shughuli mbali mbali za mazishi yake .

Mwenyekiti wa chama cha waganga wa tiba asilia (CHAWATIATA) mkoa wa Iringa Tina Mgongolwa ambaye pia ni ndugu na mwanahabari huyo anasema kuwa kwa upande wake kama mwenyekiti wa waganga mkoa wa Iringa alilazimika kuingilia kati kuwafukuza waamini wenzake nyumbani kwa mgonjwa huyo baada ya kukuta wakiendelea kumwombea bila kumpa dawa wala chakula.

Mgongolwa anasema kuwa serikali bado ina kazi nzito ya kusajili makanisa na taasisi zote zinazotoa huduma za kiroho ikiwa ni pamoja na kujua imani zake ili kuepusha vifo kwa watanzania wasio na hatia ambao wanajiunga na dini hizo.

Mwenyekiti huyo anasema kuwa dini kama hiyo hainatofauti na waganga wa kienyeji wasio waaminifu ambao wanaua watu kwa imani za kishirikiana na kuwa kuna haja ya serikali kupiga marufuku imani zinazosababisha vifo kwa watu.

Kwani anasema kitendo cha kanisa kumzuina muamini wake kunywa dawa anapoumwa ni uuaji kubwa na serikali haina budu kuwakamata viongozi wake na kuwachukulia hatua kama wanganga matapeli wanaorubuni wake kuua ili wapate utajili.

Baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini za kikristo mkoani Iringa wanasema kuwa hata wao kama viongozi wa dini bado imani za kanisa hilo zimwashtua sana na kuna haja ya serikali kuchunguza upya ujio wa kanisa hilo.

Wanasema kuwa imani ya kanisa hilo ambalo wao wanalitambua kama taasisi imekuwa ikienda kinyume na katiba ya nchi yetu inayotoa uhuru wa mtu kuabudu popote kutokana na matendo ambayo yanatendeka ni ki nyume na dini nyingine.

Mmoja kati ya waamini wa kanisa hilo na kiongozi ndani ya kanisa hilo ambaye aliomba jina lake kutoandikwa gazetini kwa kuwa si msemaji wa juu wa kanisa hilo,anasema kuwa kanisa ili mgonjwa aweze kutumia dawa lazima dawa hiyo ifanyiwe maombi kwanza vinginevyo hairusiwi kunywa dawa yoyote.

Hata hivyo anasema imani ya kanisa hilo ni ya kawaida japo wapo wanatazama tofauti kwa kuwa hawajajiunga na kanisa hilo.

Turudi katika maandiko Warumi 6;1-3 Tuseme nini basi ?Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! sisi tuliofilia dhambi sisi sote tuliobatizwa katika kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?

Mpenzi msomaji wa safu hii yawezekana kabisa kuna maswali bado hajajibwa moja kwa moja katika makala haya ,ila napenda kukuhakikishia kuwa kupitia safu hii utaweza kupata mkasa mzima wa kanisa hili na hatua ambazo uongozi wa mkoa umechukua, usikose kuungana mani wiki ijayo katika safu hii kwa mikasa mingine kama hii.

Maoni ushauri piga 0754 026 299 au 0712 750 199 pia unaweza kutembelea mtandao wa
http://www.matukiodaima.blogspot.com,ama%20www.francisgodwin.blogspot.com/

MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA