Home » » BREAKINGNEWzzzzzzzzzzzzzz GARI LA WAGONJWA LAPOTEA NA WAGONJWA ..............

BREAKINGNEWzzzzzzzzzzzzzz GARI LA WAGONJWA LAPOTEA NA WAGONJWA ..............

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, November 16, 2009 | 8:09 AM


Wakazi wa manispaa ya Iringa leo majira ya saa 7 mchana wamejikuta wakipigwa na mshangao wa mwaka baada ya Gari la kubeba wagonjwa (Ambulence) lenye namba STK 59 88 likiwa na majeruhi wawili wa ajali ya basi la Al -Asad kuwakimbiza wagonjwa ofisi za shirika la simu Tanzania (TTCL) badala ya hospitali ya mkoa wa Iringa .
Tukio hilo ambalo ni la kwanza kutokea na tukio la funga mwaka lilitokea majira ya saa 7 mchana katika eneo la Posta mjini Iringa.
Mwandishi wa mtandao huu alishuhudia gari hilo likiwa limewasha taa zote huku likipiga kwa nguvu zote king'ora kama njia ya kuomba kupishwa na magari mengine yaliyokuwa mbele ila mwisho wa yote pamoja na kupishwa dereva huyo aliwaacha wakazi wa Manispaa ya Iringa na askari wa usalama barabarani waliokuwepo eneo hilo wakishangaa baada ya gari hilo kuingia kwa mwendo wa kasi ofisi za TTCL huku likiendelea kupiga king'ora na manesi na daktari aliyekuwemo katika gari hilo akifungua milingo ya gari ili wagonjwa hao waweze kushushwa kwa matibabu .
Kutokana na wagonjwa hao kubaini kuwa wamepotea ndipo walipoamuka na kumweleza dereva huyo kuwa hapo sio hospitali ni ofisi ya TTCL na mmoja kati ya wagonjwa hao ambaye hali yake ilikuwa nafuu ndipo alipoamuka na kuanza kuelekeza njia ya hospitali ya mkoa.
Akielezea sababu ya kupotea kwa dereva huyo mmoja kati ya wagonjwa hao ambao walikuwa ni majeruhi wa ajali ya basi la Al-Asad ambalo liliparamia mlima na kujeruhi wawili katika milima ya Kitonga jana majira ya saa 6 mchana wakati basi hilo likitokea Tunduma kwenda Dar ,alisema kuwa gari hilo ni la hospitali teule ya wilaya ya Kilolo (Ilula) ila dereva wake inaonyesha ni mgeni kabisa na kama si mgonjwa huyo kutoa msaada basi yawezekana wangeendelea kuchelewa kupata matibabu kwa ugeni wa dereva huyo.
Hata hivyo alisema kabla ya kufika eneo hilo la Posta pia dereva huyo alitaka kupotea eneo la Samora ambako alitaka kuwapeleka wagonjwa barabara ya kalenga badala ya ile ya kuelekea mjini Iringa ambako ndiko hospitali ya mkoa ilipo.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA