Home » » BREAKINGNEWzzzzzzzzzzzzz RC DAR AWATIMU MGAMBO WANYANYASAJI WOTE...............

BREAKINGNEWzzzzzzzzzzzzz RC DAR AWATIMU MGAMBO WANYANYASAJI WOTE...............

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, November 2, 2009 | 7:02 AMMkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bw Wiliam Lukuvi akizindua mgambo maalum wa mkoa wa Dar leo


Kamanda wa kanda maalum ya polisi mkoa wa Dar Suleiman Kova akibariki uzinduzi wa mgambo hao

Na Francis Godwin,Dar es Salaam

SERIKALI ya mkoa wa Dar es Salaam imewafukuza mgambo matapeli ambao waikuwa wakinyanyasa watu jijini humo maarufu kwa jina la ‘Mumbamba’ kuendelea kufanya kazi hiyo ndani ya jiji hilo na badala yake kuzindua kikosi kipya cha mgambo kitakachofanya kazi katika jiji hilo kwa kuzingatia maadili ya jeshi la polisi nchini.

Mgambo hao wapya ambao wamepewa heshima ya kuwa askari wa wasaidizi wa jeshi la polisi nchini na kupewa sare maalum kwa kila halmashauri zitakazowatenganisha na mgambo matapeli pia wamepewa uwezo wa kusaidiana na askari wa usalama barabarani (Trafic ) kukamata madereva wa magari yanayokiuka sheria za usalama barabarani.

Akizindua kikosi kipya cha mgambo mchana wa leo katika viwanja vya Mnazi mmoja mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Wiliam Lukuvi alisema kuwa serikali ya mkoa huku kwa kauli moja imeridhia kuwapiga marufuku mgambo hao kuendelea kufanya kazi hiyo ndani ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam kutokana na mgambo hao kufanya kazi kinyume na maadili na wengi wao kugeuza kazi hiyo kama sehemu ya kujipatia fedha kwa kukamata magari na mali za wafanyabiashara na kuwatoza faini kinyume na taratibu .

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa katika kuondoa kero kwa wananchi wa mkoa huo ,serikali yake imeamua kuanzisha mkakati huo wa kwa kuzitaka halmashauri zote za jiji la Dar es Salaam kuingia mkabata maalum na mgambo hao ambao wamepewa mafunzi maalum ya kipolisi chini ya ufadhili wa mkuu wa polisi nchini (IGP) Said Mwema kwa ajili ya kusaidia kuliongezea nguvu jeshi la polisi na kuondoa kero kwa wananchi.

Alisema kuwa wananchi wa mko wa Dar es Salaam kwa miaka mingi wamekuwa wakinyanyashwa na mgambo hao ambao wamekuwa wakiisababishia serikali kuingia katika lawama nyingi kutoka kwa wananchi ambao wamekuwa wakitendewa ndivyo sivyo na matapeli hao ambao wamekuwa wakijipajika vyeo vya mgambo.

Lukuvi alisema kuwa mkakati huo wa kuweka mgambo maalum katika jiji hilo utaweza kukomesha vitendo vya wananchi kuendelea kusumbuliwa na mgambo hao matapeli ambao mwajiri wake ni kirungu na sare za umgambo .

“kule nchini Kenya kuna kikundi cha waharifu ambacho kimekuwa kikifanya mauwaji ya kutisha na kunyanyasa watu wasio na hatia ambacho kinaitwa Mungiki… hapa Dar es Salaam hawa mgambo matapeli ambao wamekuwa wakifunga magari ya watu na kukwamisha zoezi la kuwaondoa machinga katika maeneo yasiyo ruhusiwa tunawaita Mumbamba …..sasa nasema hawa jamaa sitapenda kuwaona hapa na atakayebainika kuchukuliwa hatua kali”

Lukuvi alisema kuwa mhambo hao maalum ambao wamesajiliwa sasa chini ya halmashauri wamepatiwa nembo maalum zinazowatambulisha na kuwa kila mgambo wa Halmashauri ya Temeke hawezi kufanya kazi katika halmashauri ya Kinondoni wala Ilala kwa mgambo atakayekutwa akifanya hivyo pia kufukuzwa kazi hiyo.

Hata hivyo aliyataka makosa 10 ambayo mgambo hao watasimamia kuyalinda yasivujwe na wananchi kuwa ni pamoja na kutupa taka ovyo ,kujisaidia barabarani na sehemu isiyo na choo, kutiririsha maji taka ovyo kutoka majumbani na sehemu nyingine, kufanyabiashara katika maeneo yasiyo ruhusiwa,kuosha na kutengeneza magari barabarani na katika maeneo yasiyo rasimi na kulaza ama kuegesha magari bila kibali .

Makosa mengine ni kubandika matangazo ovyo mitaani bila kibali cha Manispaa husika, kuuza pombe na vyakula sehemu zisizoruhusiwa ,kupiga kelele za muziki mitaani na kwenye makazi ya watu bila kibali maalum pia kufanyabiashara ya kuandaa na kuuza miwa na machungwa kando ya barabara kuu .

Hata hivyo alisema kwa wafanyabiashara wa magazeti na vijana wanaosafisha viatu wanaruhusiwa kutoa huduma hiyo popote bila kubughudhiwa.

Kwa upande wake kamanda wa kanda maalum ya mkoa wa Dar es Salaam Suleiman Kova alisema kuwa mgambo hao watafanya kazi chini ya uangalizi mkubwa wa jeshi la polisi na ndio sababu ya mkuu wa jeshi la polisi nchini kuwarejesha kazini baadhi ya makamanda wastaafu wa jeshi la polisi nchini kama aliyekuwa kamanda wa mkoa wa Dodoma Omary Mganga na wenzake kuja kusaidia serikali ya mkoa wa Dar es Salaam kutekeleza zoezi hilo.

MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA