Home » » BREAKINGNEWzzzzzzz WANAKIJIJI ZAIDI 30 KIBEBE IRINGA TABANI KWA KULA MZOGA WA NG'OMBE..........

BREAKINGNEWzzzzzzz WANAKIJIJI ZAIDI 30 KIBEBE IRINGA TABANI KWA KULA MZOGA WA NG'OMBE..........

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, November 5, 2009 | 8:12 AM

pichani mganga mkuu wa hospitali teule ya wilaya ya Iringa vijijini Dr Sabina Mangi akimhudumia mgongwa James King'unza ambaye ndiye muuzaji wa nyama hiyo ambayo ilikuwa ni mzoga.

Na Francis Godwin,Iringa

WATU zaidi ya 30 wakazi wa kijiji cha Kibebe kata ya Ulanda wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa chupu chupu wapoteze maisha huku wengine 14 wakilazwa katika hospitali teule ya wilaya ya Iringa vijijini (Tosamaganga) baada ya kula mzonga wa nyama ya ng’ombe .

Watuo hao wakiwemo 7 wa famili mbili tofauti wamelazwa katika hospitali hiyo teule ya wilaya ya Iringa huku kati yao wa wawili mama na mtoto wakiwa mahututi baada ya kucheleweshwa kufikishwa hospitali hapo.

Wakizunguza na mwandishi wa habari hizi aliyefika katika hospitali hiyo jana ,mmoja kati ya wagonjwa hao Fausta Mgongolwa alisema kuwa nyama hiyo waliuziwa kijijini hapo toka jumanne na Jumatano kutoka kwa mmoja kati ya wachuuzi wa nyama katika kijiji hicho.

Alisema kuwa baada ya kula nyama hiyo siku iliyofuata wote waliokuwa walianza kusumbuliwa na matumbo ya kuhara huku wasijue chanzo cha ugonjwa huo na baadhi yao wakijua ni ugonjwa wa kipindu pindu ama Malaria.

Hata hivyo alisema kuwa kwa ujumla wananchi wanaokadiliwa kula nyama hiyo ni zaidi ya 30 kutokana na mfanyabiashara huyo wa nyama na wenzake kijijini hapo kuwa na wateja wengi zaidi.

Alimtaja muuzaji wa nyama hiyo kuwa ni James King’unza (42) mbaye pia amelazwa na familia yake hospitalini hapo.

Mganga mkuu wa hospitali hiyo Dr Sabina Mangi alisema kuwa wagopnjwa hao wamefikishwa leo majira ya saa 9 alsiri na kuwa hadi majira ya saa 11 jioni wagonjwa 14 ndio ambao walikuwa wamekimbizwa katika hospitali hiyo.


Aliwataja waliolazwa kuwa ni Subira Kihaga (27), Ragina King’unza (30), Habiba Lugakila (mtoto wa miezi 10), Fausta Mgongolwa (41), James King’unza(42), Peter Kalongole(57),Linusi Kunzugala(59), Mwandisabu Kalongole( 9) na Juma Kyega (9).

Wengine ni Victor Kalongole (4.6),Majima Kinunza(6),Debora Kalongole(21),Rosina Waya(40) na Saida King’unza (3.6).

Aliwataja wagonjwa wawili ambao hali zao ni mbaya zaidi kuwa ni Rosina Waya (40) pamoja na mtoto wake wa miaka 3na miezi 6 Debora kalongole.

Huku wagonjwa saba kati yao akiwemo James King’unza , Habiba Lugakila, majina King’unza, Ragina King’unza, Subira Kihaga na Fausta Mgongolwa hali zao zinaendelea vizuri pamoja na kuendelea kutapika na kuharisha mara kwa mara.

Mganga huyo alisema jitiahada za waganga katika hospitali hiyo zinaendelea ili kunusuru maisha ya wagonjwa hao .

Dr Mangi alisema kuwa bado hadi sasa haijafahamika aina ya sumu iliyokuwemo katika mzoga huo ambayo imesababisha afya za wakazi hao kwenda vibaya zaidi na kuwa timu ya madaktari kutoka hospitali ya mkoa wa Iringa wamekwenda kijijini ili kupima mzoga huo.

MWISHO


Waweza kusoma habari hii katika gazeti la Tanzania Daima kesho
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA