Home » » BREAKINGNEWzzzzzzz MAJAMBAZI WATEKA MAGARI WAJERUHI KWA MAPANGA NYANG'ORO LUKUVI NA WAANDISHI WANUSURIKA KUTEKWA...............

BREAKINGNEWzzzzzzz MAJAMBAZI WATEKA MAGARI WAJERUHI KWA MAPANGA NYANG'ORO LUKUVI NA WAANDISHI WANUSURIKA KUTEKWA...............

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, November 24, 2009 | 9:15 AMWATU watano wanaosadikika kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za jadi kama virungu na mapanga wameteka malori mawili na kumewajeruhi kwa mapanga abiria na kisha kuwapora fedha na simu wafanyabiashara wa samaki waliokuwa wakitoka kufunga mali katika bwawa la Mtera Iringa .(pichani ni kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Evarist Mangalla)

Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 2.30 usiku muda mfupi baada ya msafara wa mbunge wa jimbo la Ismani na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bw Wiliam Lukuvi kupita katika milima hiyo ya Nyang’oro akitokea kuzindua ujenzi wa soko la kimataifa la Samaki linalojengwa katika jimbo lake eneo la Migori –Mtera.

Wakielezea kuhusiana na tukio hilo la utekaji magari abiri waliokuwemo katika malori hayo walisema kuwa wakati tukio hilo likitokea magari matatu likiwemo la mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Fundi Mihayo ambalo lilikuwa na waandishi wa vyombo mbali mbali vya habari akiwemo mwandishi wahabari hizi ,gari la mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Bi.Tina Sekambo na gari la mbunge Lukuvi yalikuwa yamepita katika milima hiyo kama nusu saa iliyopa.

Walisema jameruhi hao kuwa msafara wa mbunge huyo ulikuwa umewapita katika kijiji cha Izazi ambako wao walikuwa wamesimama kupata chakula na majira ya saa 2 hivi ndipo walipoanza safari katika milima hiyo kuelekea mjini Iringa.

Hata hivyo baada ya kufika katika kona za milima hiyo ya Nyang’oro ndipo walipopatwa na wakati mugumu baada ya kuona magogo yametegwa kati kati ya barabara na kuyafanya magari hayo kusimama kutokana na kukosa kwa kupita na ndipo majambazi hayo zaidi ya watano walipojitokeza kutoka msituni wakiwa na mapanga na marungu na kuwataka abiria wote kushuka na kulala chini .

Walisema abiria wa malori hayo Bw John Ndelwa na Salome Kalinga kuwa malori hayo yalikuwa na abiria zaidi ya 20 hivi na baadhi ya abiria ambao ni wafanyabiashara walionesha jeuri na kugoma kulala chini na ndipo majambazi hao walipoamua kuwalazimisha kulala chini kwa kuwakata mapanga.

Mbali ya kuwakata mapanga baadhi ya wafanyabiashara pia majambazi hao walitumia fimbo kuwaadhibu abiria hao walitekwa na kuwataka kutoa fedha na simu za viganjani.

Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Bw Claus Mwasyeba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kuyataja magari yaliyotekwa kuwa ni gari namba T 153 APB Fuso mali ya Hezrony Byaton wa Makambako Njombe lililokuwa likiendeshwa na Maneno Kisogo (25) mkazi wa Makambako wilaya ya Njombe na gari namba T 558 AFY fuso mali ya Eliawani Chau mkazi wa Kihesa Iringa lililokuwa likiendeshwa na Elioni Chau (26) mkazi wa kihesa Iringa mjini.

Alisema kuwa majambazi hao watano walikuwa na nondo,mapanga na marungu na kuwa wanadaiwa kupora fedha kiasi cha shilingi milioni 4.5 pamoja na simu 12 kutoka kwa wafanyabiashara hao ambao wengi wao ni wafanyabiashara wasamaki na barafu.

Aliwataja waliojeruhiwa katika tukio hilo na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa kwa matibabu kuwa ni Sereman Sanga (28),Honh Kiunge(39), Mashauri Mapenze (28) na Thomas Mapenze (55).

Kaimu kamanda huyo alisema kuwa jitihada za jeshi la polisi mkoani Iringa kuendelea kuwasaka majambazi hao zinaendelea kufanywa kwa kushirikiana na wananchi wanaozunguka eneo hilo .

Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Iringa Dr.Oscar Gabone alithibitisha kupokea majeruhi hao na kuwa wote walipatiwa matibabu na kuruhusiwa .

Habari hii imeandikwa na Francis Godwin mwandishi wa habari za gazeti la Tanzania Daima mkoa wa Iringa na itachapwa katika gazeti hilo kesho
MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA