Home » » BRAEKINGNEWzzzzzzzzzzzzzzzz MUUZA NYAMA ANUSURIKA KIPIGO KWA KUGOMA KUONJA NYAMA

BRAEKINGNEWzzzzzzzzzzzzzzzz MUUZA NYAMA ANUSURIKA KIPIGO KWA KUGOMA KUONJA NYAMA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, November 17, 2009 | 5:54 AM


(Pichani ni ;Abiria na wafanyabiashara wa nyama wakitoka kushuhudia muuza nyama eneo hilo ambaye alikuwa amekabwa koo kwa kugoma kuonja nyama huku katikati ni jiko la muuzaji huyo likiwa limetolewa nyama na kutupwa katika shimo la taka)

Na Francis Godwin, Mvomero

Abiria waliokuwa wakisafiri na basi la Tonda kutoka Mbeya kwenda jijini Dar e Salaam leo wametaka kutembeza kipigo kwa mmoja kati ya wafanyabiashara wa nyama katika eneo la Soko la Miwa ,Kipera wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro baada ya mteja mmoja kushitukia nyama hiyo kuwa si ya ng'ombe ,mbuzi wala kondoo na kumataka muuzaji huyo kuonja kwanza .

Tukio hilo lilitokea majira ya saa 8.05 mchana katika eneo hilo umbali wa Km 20 kutoka mjini Morogoro ambalo ni maarufu kwa nyama choma .

Abiria huyo aliyejitambulisha kwa jina la Kevin Kyando alisema kuwa amechukua uamuzi wa kumtaka muuzaji huyo kuonja nyama hiyo baada ya kubaini kuwa nyama hiyo si nyama ya mbuzi kama alivyomueleza wakati wa kumuuzia .

"Hivi wana jamaa wanataka kuendelea kutulisha mbwa hadi lini ....kwani mimi ni mtaalam sana wa nyama ...ila hii si nyama ya mbuzi ,wala kondoo japo muuzaji alinieleza kuwa ni nyama ya mbuzi ila baada ya kumuuliza tena aligeuza kuwa ni nyama na kondoo mara nyama ya ng'ombe ....sasa ni ng'ombe gani mwenye miguu mwembamba kama mbuzi kama sio kaniuzia mbwa huyo ...kweli kama kweli nyama ya kweli kwanini bei iwe maelewano yaani 2000 ama 1500 hadi 1000" alihoji huku akiwa amemshika kijana huyo .

Hata hivyo kutokana na basi hilo kuwa mbioni kuondoka abiria huyo alilazimika kumwachia kijana huyo huku akitaka kurejeshewa fedha zake kiasi cha shilingi 2000 alizokuwa ametoa kwa ajili ya kulipia kitoweo hicho .


Kwa upande wao abiria wakizungumzia eneo hilo walisema kuwa kimsingi serikali ya mkoa wa Morogoro inapaswa kutupiwa lawama zote kwani wafanyabiashara hao wapo siku zote na hakuna bwana afya anayefika kupima nyama hiyo na kuhakikisha kuwa ni mbuzi ama ng'ombe.

Walisema kuna uwezekano mkubwa wasafiri wamekuwa wakilishwa mizoga na mbwa bila wao kujijua jambo ambalo linapaswa kuchunguzwa na serikali ya wilaya ya Mvomelo pamoja na mkoa huo .

"eneo hili ni porini kabisa hivi nyama hii inapimwa na nani na kweli ni nyama ya mbuzi ?na kama mbuzi kwanini muuzaji aligoma kuonja huku akikimbia ? .....wengi tumekuwa tukila mbwa bila kujijua ...sasa kuanzia leo sitajaribu tena kula nyama katika eneo hilo la soko la miwa bora kwenda kula hoteli ambako ni uhakika wa vyakula vinavyouzwa hapo"


Habari za uhakika kutoka kwa viongozi wandamizi wa wilaya ya Mvomero zinadai kuwa wafanyabiashara hao walipigwa marufuku kwa zaidi ya miaka miwili iliyopita na aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo Bi.Hawa Ng'humbi ambaye kwa sasa amehamishiwa wilaya ya Makete mkoa wa Iringa .

Jitihada za kumtafuta mkuu wa wilaya ya Mvomero Bi. Fatma Mwasa zinaendelea kufanywa na mtandao huu ili kujua sababu ya wilaya kuruhusu biashara katika eneo hilo bila kuwepo kwa wathibiti wa afya.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA