Home » » B

B

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Wednesday, November 11, 2009 | 3:46 AM

Na Francis Godwin,Iringa

UMATI mkubwa wa wananchi wa Manispaa ya Iringa wakiwemo baadhi ya ndugu wa marehemu wa ajali ya gari lenye namba za usajili T 789 AFN Isuzu Forward (Lori ) lilopata ajali juzi Kihesa mjini hapa leo wamefurika katika mahakama ya hakim mkazi wa wilaya ya Iringa kusikiliza kesi ya dereva wa gari hilo Edward Mwendele (47) mkazi wa Muungano Frelino mjini Iringa ambaye alifikishwa kwa mara ya kwanza kusomewa mashtaka yake.

Pamoja na umati huo kufika mahakamani hapo kutaka kushuhudia zoezi la kusomewa mashtaka bado dereva huyo aliwashangaza wananchi hao pale alipotaka kuvua nguo mbele ya mahakama kwa lengo la kumwonyesha majeraha katika mwili wake ili hakimu huyo aweze kumwonea huruma na kumwachia kwa dhamana.

Mtuhumiwa huyo alifanya kituko hicho baada ya mwendesha mashtaka wa polisi Inspecta Leonard Tungalaza kumaliza kumsomea makosa yake 9 na kuiomba mahakama hiyo kuto toa dhamana kwa sasa kwa mtuhumiwa huyo kutokana na usalama wake kutoka kwa ngudu wa marehemu ambao wengi wao bado wanajazba kwa kupoteza ndugu zao.

Awali mwendesha mashtaka huyo wa polisi alisema mtuhumiwa huyo Novemba 9 majira ya jioni mwaka huu katika eneo la Kihesa mjini Iringa aliendesha gari lake kwa uzembe mkubwa na kusababisha vifo vya watu watano na wengine wanne wakijeruhiwa .

Hivyo aliieleza mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa huyo anakabiliwa hayo ambayo ni ya kiusalama barabarani likiwemo la kuendesha gari hilo kwa uzembe na kuvamia makazi ya watu kwa kugonga nyumba hiyo na kusababisha vifo hivyo na majeraha kwa watu hao .

Hata hivyo mtuhumiwa huyo alionyesha kutaka kukubali kosa moja la kuendesha kwa uzembe na kuvamia makazi ya watu na kugonga nyumba na kusababisha majeraha kwa abiri wake Adam kapela kabla ya kuiomba radhi mahakama hiyo kuwa alisahau kama makosa mengine ameyakana na hivyo na hilo lijulikane kuwa na si kweli.

“Sahamani mheshimiwa hakimu ….kwa kuwa makosa yote nimekataa hata hilo nililotaka kukubali naomba kulikana kuwa si kweli….ila naomba tu mahakama itazame majeraha hayo (huku akivua shati lake )…mimi naumwa sana hapa nilipo najifanya kujikaza tu kweli naomba mahakama inionee huruma niweze kwenda nyumbani kutibiwa” aliomba mtuhumiwa huyo.

Kuwa tangu apate majeraha ni sindano moja pekee ndio ambayo amechomwa hivyo bado anaumwa sana kwa tukio hilo la ajali.

Kwa upande wake hakimu wa mahakama hiyo Selfu Kulita alisema kuwa mahakama yake imezingatia maombi yaliyotolewa na mwendesha mashtaka huyo wa jeshi la polisi ya kutaka mtuhumiwa huyu kutopewa dhamana kwa sasa kwa ajili ya usalama wake.

Hivyo alisema kutokana na huduma za matibabu kuwepo mahabusu ,mahakama yake imekubali mtuhumiwa huyo kurudi mahabusu hadi Novemba 25 mwaka huu ambapo kesi hiyo itatajwa tena .

Huku kuhusu dhamana ya mtuhumiwa ambayo kwa kesi hiyo dhamana yake ipo wazi ,mahakama itajadili upya katika kikao chake hivi karibuni.

MWISHO

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA