Home » » RAIS KIKWETE AIZINDUA WILAYA YA KILOLO...............

RAIS KIKWETE AIZINDUA WILAYA YA KILOLO...............

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, October 27, 2009 | 11:37 AM

Na Francis Godwin,Iringa

RAIS Jakaya Kikwete leo amezindua makao makuu ya wilaya ya Kilolo mkoani Iringa na kuipongeza halmashauri ya wilaya hiyo kwa ujenzi wa jengo la ghorofa la kisasa kwa ajili ya halmashauri ya wilaya hiyo jengo ambalo limejengwa kwa gharama nafuu ukilinganisha na halmashauri nyingine nchini ambazo zimejenga majengo madogo kuliko hilo kwa gharama kubwa.

Akiwahutubia mamia ya wananchi wa wilaya ya Kilolo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo mara baada ya kuzindua miradi mitatu ukiwemo wa umeme,jengo la halmashauri na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kilolo,Rais Kikwete alisema kuwa kwa upande wake amefurahishwa na uaminifu mkubwa wa halmashauri hiyo katika kusimamia fedha za serikali kwenye ujenzi wa majengo hayo.

Rais Kikwete alisema zipo halmashauri ambazo zimejenga majengo madogo kuliko hayo ila ukitazama gharama zilizotumika ni kubwa kuliko gharama zilizotumika kujenga jengo hilo la halmashauri ya wilaya ya Kilolo ambalo ni jengo la kisasa ukilinganisha na majengo yaliyojengwa katika halmashauri nyingine kwa gharama kubwa.

"Kweli halmashauri ya Kilolo pamoja na makandarasi na wataalam wengine wote mlio shiriki kujsimamia ujenzi wa jengo hilo napenda kuwapongeza sana kwa uaminifu mkubwa mlioonyesha katika ujenzi wa jengo hilo....nasema nawapongezeni sana"

Rais Kikwete alisema kuwa ujenzi wa makao makuu ya wilaya ni moja ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ambao iliahidi kuwa miundo mbinu yote ya makao makuu ya wilaya kujengwa kisasa kabla ya mwaka 2010 kazi ambayo utekelezaji wake umekuwa ukifanywa kwa nguvu zote.

Hata hivyo alisema kuwa huduma kubwa katika halmashauri hiyo ni hospitali ya wilaya ambapo mbali ya kuwa katika wilaya hiyo ipo hospitali teule inayofanya kazi kwa ushirikiano na kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ila bado serikali ina mpango wa kujenga hospitali ya serikali.
Rais Kikwete alisema kuwa kuanzisha wilaya bila kuwa na huduma za kijamii kama ofisi na ubora wa miundo mbinu ni sawa na kuwabebesha wananchi mbuzi katika gunia.


Awali mkurugenzi mtendaji wa halamshauri ya wilaya ya Kilolo Bosco Ndunguru alisema kuwa jengo hilo lina ofisi 56 ,stoo 4 ukumbi mkubwa mmoja ,kumbi ndogo 2 pamoja na vyumba vingine vingi limewajali watu wenye ulemavu pia kwa kuwatengea maeneo yao.

Alisema kuwa makisio ya ujenzi huo yalifanywa mwaka 2006 /2007 ambayo yalikuwa ni shilingi 2,321,004,000 huku ujenzi halisi utagharimu shilingi 2,005,199,468
Bofya hapa
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA