Home » » WAZIRI MWANGUNGA AFUNGA GHAFLA MAONYESHO YA UTALII IRINGA ..................

WAZIRI MWANGUNGA AFUNGA GHAFLA MAONYESHO YA UTALII IRINGA ..................

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, September 28, 2009 | 7:44 AM


Mzee Mwaruaha ambaye ni mkurugenzi wa mkaa wa Moto moto akisalimiana na waziri wa utalii na maliasili Shamsa Mwangunga leo baada ya kufurahishwa na ubunifu huo wa mkaa wa moto moto ,pembeni ni Rajani Mwaruaha


Waziri wa utalii na maliasili Shamsa Mwangunga (kushoto) akiwa amekaa na mzee wa kihehe Gerady Malangalila leo kabla ya kufunga maonyesho ya wiki ya utalii mjini Iringa
Na Francis Godwin,Iringa

MAADHIMISHO ya wiki ya utalii ambayo yalipaswa kufikia kilele chake kesho ( jumanne) yamefungwa ghafla leo na waziri wa maliasili na utalii Shamsa Mwangunga huku kukiwa na mkanganyiko kubwa katika ufungaji wa maadhimisho hayo baada ya kuwepo kwa ratiba mbili ikiwemo inayoonyesha mgeni rasimi ni katibu mkuu kiongozi Philip Luhanjo na ile inayoonyesha waziri huyo .

pamoja na mkanganyiko huo pia mmiliki wa hoteli ya kitalii ya Kalenga Westpark Bw Juma Kaundama pia aligoma kuzindua hoteli yake kwa ratiba ya kushitukiza baada ya kupewa masaa takribani saba ya kufanya maandalizi kabla ya waziri ama katibu mkuu kupitia kuzindua jengo la hoteli hiyo lililopo Miyomboni.

Katika ratiba ya kwanza iliyotolewa na kamati ya maandalizi ya sherehe hizo ambayo mwandishi wa habari hizi pia ana nakala yake iliyonyesha kuwa waziri Mwanguka angepita kufungua hoteli hiyo majira ya saa 8.30 hadi 9 ;00 alasiri kabla ya kuelekea uwanja wa maonyesho kwa ajili ya kuhitimisha maadhimisho hayo.


Huku ratiba ya pili ambayo mwandishi wa habari hizi aliipata kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Iringa Mohamed Abdulaziz ambayo nayo nakala yake ipo ,ilionyesha kuwa mgeni rasimi katika maadhimisho hayo ni katibu mkuu kiongozi Luhanjo ambaye pia alipangiwa kukagua hoteli hiyo ya kalenga majira ya saa 8 mchana hadi saa 9 alasiri

Pamoja na kuwepo kwa mgongano wa nani kuwa mgeni rasimi katika ufungaji wa dharula wa maonyesho hayo bado msafara wa waziri wa maliasiri na katibu kiongozi ulionekana kufika kwa pamoja katika viwanja wa Samora katika ufunguji wa maadhimisho hayo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na kutofunguliwa kwa hoteli hiyo ya kalenga mkurugenzi wake Kaundama alisema kuwa ameshindwa kuruhusu waziri kufungua hoteli hiyo kama ilivyopangwa kutokana na kuwepo kwa mwingiliano wa ratiba na kuwa awali yeye aliomba kwa uongozi wa mkoa kuwa wiki kiongozi wa kitaifa ambaye angefika kwenye maonyesho hayo kumsaidia kufungua hoteli yake pia ila hadi juzi majibu yalikuwa hayajatolewa .

"Mimi nilijua imeshindikana baada ya kuwaomba kwa zaidi ya siku nne sasa ila sikupata jibu na leo (jana) asubuhi ndipo naletewa ratiba kuwa hoteli yangu itakuwa kwenye ratiba ya kuzinduliwa jambo ambalo kwangu lilikuwa gumu kutokana na kutokuwepo kwa maandalizi yeyote ya kufungua hoteli hii"

Alisema kaundama kuwa alilazimika kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa na kumwomba kusogezewa mbele ufunguzi huo hadi atakapofanya maandalizi upya.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Abdulaziz akizungumzia kuhusu mkanganyiko wa ratiba hiyo alisema kuwa maadhimisho hayo yamefungwa jana kutokana na mwingiliano wa ratiba alionao waziri na kuwa hata hoteli hiyo itapangiwa muda na kiongozi mwingine wa kuzindua.
kupata matukio ya mwanzo bonya hapa
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA