Home » » RC IRINGA ALIVYOPONEA KATIKA TUNDU LA SINDANO KUJLA SAHANI MOJA NA MATAPELI MAKETE..............

RC IRINGA ALIVYOPONEA KATIKA TUNDU LA SINDANO KUJLA SAHANI MOJA NA MATAPELI MAKETE..............

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, September 25, 2009 | 8:49 AM


Na Francis Godwin,Iringa

MKUU wa mkoa wa Iringa (RC) Mohamed Abdulaziz (pichani)leo amegoma mwaliko wa kuwa mgeni rasimi kwa ajili ya kuchangisha michango ya ujenzi wa Mabweni katika shule za sekondari wilayani Makete baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu mkubwa katika taasisi hiyo isiyo kuwa ya kiserikali (NGOs) ambayo inatumia jina la wilaya ya Makete kuchangisha bila kuwa na usajili wala viongozi wa wilaya hiyo kupewa taarifa.

Pamoja na kugoma kufika kufungua harambee hiyo iliyokuwa ifanyike katika hoteli ya M.R mjini Iringa pia ameipiga marufuku NGOs ijulikanayo kama Co .Operation For Assistinga Handicapped People Tanzania yenye makaa yake makuu jijini Dar es Salaam kufanya harambee hiyo hadi itakapoonyesha vibali vyake za usajili.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake baada ya kunusurika kuingiwa mjini na NGOs hiyo ya mfukoni mkuu wa mkoa alisema kuwa alipokea barua kutoka kwa mkurugenzi wa NGOs hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Shengena ila baada ya kufanya uchunguzi zaidi jana kabla ya kwenda kushiriki harambee hiyo aliamua kufanya mawasiliano na mkuu wa wilaya ya Makete na mkurugenzi wake ili kujua wilaya imeshiriki vipi katika suala hilo .

"Kweli ajabu kwani mkuu wa wilaya nilipo muuliza juu ya NGOs hii alisema hajui chochote na wala hakuna shughuli yoyote ya wilaya yake inayofanyika mjini Iringa...huku mkurugenzi naye akikataa kuitambua NGOs hiyo ambayo inataka kujenga mabweni ya kisasa katika shule za sekondari bila wilaya kujua wala walimu wa shule husika"

Mkuu wa mkoa alisema kuwa baada ya wilaya kuonyesha kutoitambua NGOs hiyo alimwita mkurugenzi wa NGOs hiyo na kumtaka aonyeshe kibali cha usajili wa NGOs yake ama barua inayomruhusu kufanya harambee vyote hakuna navyo.

Hata hivyo alisema kuwa kabla ya kutaka kufanya harambee hiyo Iringa pia mkurugenzi wa NGOs huyo ambaye anafanya kazi zote peke yake aliwahi kuhojia katika kipindi cha jambo Tanzania TBC 1 asubuhi moja ambapo alieleza nia ya kutaka kuja Iringa kufanya harambee hiyo.

Alisema kuwa katika hali ya kushangaza NGOs hiyo kamati nzima inaundwa na mkurugenzi mwenyewe hali ambayo inaonyesha wazi kuwepo kwa dalili za ubabaishaji mkubwa .

Aidha uchunguzi uliofanywa na ofisi yake alisema kuwa umebani kuwa NGOs hiyo iliwahi kuandaa matembezi jijini Dar es Salaam na kumwalika waziri wa maendeleo ya jamii jinsi na watoto Margaret Sitta ambaye alimtuma katibu mkuu wake ambaye pia alikataa kwenda huko kutokana na kutoitambua vyema NGOs hiyo.

Hata hivyo mkuu wa mkoa alisema kuwa hakatazi NGOs kuja kufanya kazi Iringa hasa wilaya ya Makete na wilaya nyingine za mkoa wa Iringa ila kabla ya kuja kufanya kazi lazima taratibu zifuatwe ili kuwepo kwa uratibu mzuri wa michango ya wananchi na wahisani .

Hata mkurugenzi wa NGOs hiyo alipotafutwa na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu ili kuweza kutolea ufafanuzi juu ya uhalali wa NGOs yake hiyo hakuweza kupatikana kabisa.
MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA