Home » » MWAMOTO ATOA KAULI NZITO KWA MBUNGE MSOLLA KILOLO...............

MWAMOTO ATOA KAULI NZITO KWA MBUNGE MSOLLA KILOLO...............

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, September 27, 2009 | 11:01 AM

Na Francis Godwin,IringaALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Venance Mwamoto amempongea mbunge wa jimbo hilo Profesa Peter Msolla ambaye ni waziri wa mawasiliano Sayansi na Teknolojia kuwa amefanya jitihada kubwa katika maendeleo na kuwawataka wananchi wote wa jimbo hilo kumuunga mkono Mbunge na kuwa kwa upande wake ataendelea kushirikiana naye .

Alitoa kauli hiyo jana kwenye sherehe za kumsimika Prof Msolla kuwa kamanda mpya wa UVCCM wilaya ya Kilolo nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Mwamoto kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita .


Mwamoto alisema huu si wakati wa kuvutana kisiasa wala kuendekeza makundi ndani ya chama na badala yake wananchi wote kuungana na kuwa pamoja na mbunge huyo ili kuhakikisha mambo ya kimaendeleo katika wilaya hiyo yanakwenda kama kawaida na kuwa iwapo mbunge wa sasa atashindwa kutekeleza yale aliyokusudiwa basi atapokelewa nafasi hiyo.


"Siasa sio ugomvi mimi na Msolla ni mtu na shemeji yake hivyo hakuna ugomvi hapa ili wote tunagombea kuwaletea wananchi maendeleo na kuwa uongozi ni sawa na mbio za vijiti ambazo lazima kupokezana na kuwa pale atakaposhindwa kutimiza wajibu wake basi mbunge atapokelewa nafasi hiyo."


Prof Msolla alisimikwa ukamanda huo na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Deo Sanga ndiye katika sherehe iliyohudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Kilolo, Sethy Mwamotto, mamia ya wafuasi wa CCM wa wilaya hiyo, wawakilishi wa vijana kutoka wilaya zote za mkoa wa Iringa, viongozi wa chama na serikali wa wilaya ya Kilolo na mkoa wa Iringa zilifanyika juzi katika uwanja wa michezo wa Ilula, wilayani Kilolo.

Mbali na kupata kuwa mbunge, Mwamotto ndiye aliyekuwa kamanda wa umoja huo kwa miaka kumi iliyopita.

Mwamotto alisema amelazimika kukubali dhana ya uongozi wa kupokezana vijiti hivyo si sahihi kuruhusu malumbano ya kisiasa yaendelee jimboni humo.

Aliwataka wanaCCM wa jimbo hilo kutowaruhusu wageni kuwagombanisha na kumsamehe kama kuna jambo lolote alilifanya na likawakwaza wana CCM kwa ujumla wao.

Akishukuru kwa ushirikiano anaopata kutoka kwa wananchi wa jimbo la Kilolo, Prof Msolla alisema jumuiya ya vijana ndani ya chama hicho ni muhimu sana hivi sasa kuliko ilivyokuwa wakati wa utawala wa chama kimoja.

Alisema katika kipindi cha miaka mitano ijayo atakachokuwa kamanda wa umoja huo katika jimbo atahakikisha umoja huo unaimarika na unakuwa na mikakati itakayowafanya wasiwe ombaomba.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA